Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

SAMATTA ATUMIKE KAMA DARAJA KWA WACHEZJI NA VILABU NCHINI

Samatta 77
Na Dastan Nehemia

Usajili wa Mbwana Samatta kutoka TP Mazembe kwenda KRC Genk ya Ubeligiji ni hatua nzuri kwa wachezaji chipukizi wa Tanzania na vilabu vya soka kutumia usajili huu wa Samatta kama daraja na kuvuka na kwenda mbele kisoka.


Mbwana Samatta baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za Afrika ni hatua kubwa kwani vilabu vikubwa duniani sasahivi macho yao yako nchini kutazama wachezaji wengine, ndio maana hata Thomas Ulimwengu amekuwa akiwindwa na vilabu vingi hii ni kutokana na Samatta kufungua njia.


Vilabu vikubwa duniani huamini mchezaji mmoja bora anapopatikana kutoka nchi fulani huwa kuna wengine zaidi ya mia moja nyuma yake ni kama mgodi wa madini hauwezi hutoa almasi moja tu lazma ziwepo nyingine na ni kama kwenye muziki wa kizazi kipya baad ya diamond Plutnumz kuanza kupata tuzo za kimataifa njia pia zimefunguka kwa wasanii wengine kama Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz kupa tuzo za kimataifa pia.


Juhudi zikiongezeka kwa wachezaji baada ya mwaka mmoja tu tusishangae kuona chipukizi kama Haji Ugando, Hassan Kessy, Ramadhani Singano (Messi) na Haji Mwinyi wakiwa Italia au Ubeligiji wakicheza mpira katika klabu mojawapo.


Jambo la msingi ni vilabu vyetu vya hapa nchini kujifunza kutoka kwa klabu kama TP Mazembe ambayo imefanya uwekezaji wa kweli na inaongozwa na viongozi makini wa soka na ndiyo maana inafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na hiyo ndiyo sababu inayopelekea wachezaji wao kupata kuonekana na vilabu vya Ulaya.


TP Mazembe kwa kumuuza Mbwana Samatta kwenda kwenda KRC Genk waamepokea Tsh billion 1.6 pesa ambayo ingepata moja vilabu vya Tanzania ingesaidia katika uwekezaji hasa ujenzi wa viwanja vyao binafsi na kusaidia kuongezeka upatikanaji wa mapato.


Endapo vilabu vyetu vya Azam FC, Yanga SC na Simba SC, vilabu ambavyo vinasemekana vinawachezaji bora vikipata nafasi ya kufanya vizuri kwenye klbu bingwa Afrika na kombe la shirikisho basi wachezaji wa kitanzania watapata nafasi kuonekana na kununuliwa na klabu kubwa za Ulaya hili litasaidia kukuza soka letu na kutengeza timu nzuri ya taifa.


Lakini je vilabu vyetu vya Simba na Yanga vinapigania wachezaji kutoka kwenda kucheza Ulaya?


Sababu mara nyingi tumekua tukiona hivi kwa matakwa yao binafsi vikiwanyima fursa wachezaji wao kujiunga na vilabu vikubwa, lakini endapo wangetambua umuhimu wa wachezaji hawa kwenda vilabu vikubwa basi vilabu vyetu vingekua vikipigana kuwapeleka wachezaji wao kufanya majaribio mara kwa mara kama vilabu vya Afrika Magharibi nchi kama Nigeria, Ghana na Senegal kucha kutwa wanapeleka wachezaji wao nchi za Ufaransa, Italia, Ubeligiji na Uholanzi kufanya majaribio katika vilabu mbalimbali kwa gharama zao.


Hivyo basi watanzania tusisherekee tu Mbwana Samatta kwenda Ulaya bali tumtumie kama daraja la kupitia wachezaji wengine.


0655995405
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top