Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

NAY WA MITEGO AMPA POLE WEMA SEPETU

Msanii wa muziki wa Hip Hop Nay wa Mitego amesema hakupenda ujauzito wa Wema Sepetu uharibike kama baadhi ya mashabiki wa Wema Sepetu wanavyodai katika mitandao ya kijamii.
nay new2

Rapa huyo kupitia wimbo wake “Shika Adabu Yako’ alimchana Wema ‘una mimba kweli, au ndio kiki za msimu?. Miezi tisa sio mingi, isije ikakugharimu” kauli ambayo ilitafsiriwa vibaya na mashabiki wa Wema.

Akizungumza katika kipindi cha Ubaoni cha EFM Jumatano hii, Nay alisema yeye hawezi mwombea mabaya Wema kwa kuwa anapenda sana watoto.

“Sijapenda ujauzito wa Wema uharibike kwani napenda watoto. Kama ilikuwa mimba kweli nampa pole sana dada yangu ila kama ilikuwa kiki imefika mwisho Kwani nilichoongea kwenye wimbo ilikuwa ni swali Je? Una mimba kweli au drama.,”alisema Nay.

Mange Kimambi Afunguka, Atoa Ushauri Kwa Wema Sepetu Baada ya Kusemekana Mimba Kutoka...


From Mange Mange kimambi_

"Baada ya kusoma posti ya Idris all I can say is Pole mdogo wangu.
Kama hukuwa na mimba kama wasio kupenda wanavyodai au kama kweli ulikuwa nayo ni wewe, Idris na Mungu mnaeujua ukweli. Wanawake wengi mno wanapata miscarrage especially mimba ya kwanza, ila kwako wewe lazma waseme ulikuwa unatafuta Kiki. Like is said ukweli mnaujua wenyewe.
Wema wewe sio mtu kuchukua ushauri ila this time naomba uchukue ushauri wangu pls. Theres a reason why wanawake huwa wanaambiwa hata na madoctor wasitangaze mimba mpaka ipite 4 months and thats because mimba chini ya miezi minne inaweza kutoka anytime. Hata dadako hapa huwa nakuwa na kiherehere cha kutangaza kwenye blog nna mimba ila huwa najikaza mpaka niingie 2nd trimester.
Next time news kama hizi only share with your mom na dada zako not marafiki . Kumbuka hizi habari zilianza kutanganzwa na marafiki zako , i think baada ya hapo na wewe ndo ukapata mshawasha wa kutangaza. Hao sio rafiki zako Wema hakuna rafiki anaweza kumtangazia rafiki yake anaempenda kimimba cha mienzi miwili ,huo ni wakati wa kuomba kwa Mungu mimba ikue na ikomae na sio muda wa kutangazia wajinga. Mimi personally nilitaka hata kulia ulipotangaza but it was too late.

Another thing Wema, hivi kwanini unakubali kuwa pressured na wajinga wa social media kuzaa when you are not ready??? The pressure is getting to you Wema. Mbali na familia yako ni mimi peke yangu ndo ninae jua umri wako Wema, Wema huna hata 26 years we mtoto. toka lini mtu mdogo hivyo akawa classified as tasa??? Why unakubali kupewa pressure uzae ukiwa mdogo hivi? hata kuolewa hujaolewa?? Achana nao mdogo wangu, acha waongeee midomo mali yako. Subiri uolewe ndo uzae ,hujawahi hata kuishi na mwanaume for more than a year why uitwe tasa na wewe uanze kupata mshawasha wa kubeba mimba? Achana na hao wapuuzi. Mwishowe uje kuzaa mtoto while you are not ready au uzae na mtu huna mpango wa kuishi nae kisa tu uwakomeshe hawa wajinga wa kwenye mitandao. utajikomesha mwenyewe. Please dont succumb to the pressure. You are way too young.

Wanakushindanisha na wanawake ambao unatakiwa uwaamkie tena kwa kupiga goti na wewe unakubali kabisaaa. Kuzaa wanazaa mpaka panya when the time is right utazaa.

Another thing, don't succumb to the pressure ya maisha ya ex wako. Kama Kweli uliwahi kumpenda be happy for him that he is happy! That's what love is! Na wewe you will be happy. Usipewe pressure na hawa mbwa wa kwenye mitandao kuwa your ex is happy with so and so mpaka Na wewe uwe Na pressure ya kuwa na Mtu. Au kukufanya Na wewe uanze kuonyesha uko in love na Mtu. You are a beautiful woman you can pull any man you want. Take your time pls! Hawa mbwa wa kwneye mitandao wanaweza kukufanya ukaharibu Maisha yako ili uwa prove wrong. Achana nao. .

Listen everything happens for a reason. Kuna Sababu maalum why wewe Na Diamond hamko pamoja and that's because kuna mwanaume Mungu amekupangia. Labda ushakutana nae maybe not but yupo wa kwako.

Mi Naomba uwe Kama Beyoncé , her love life is soooooo private Mpaka haters wanakosaga cha kusema. Be private na wanaume maboyfriend and so forth. Ukiolewa Au ukichumbiwa ruksa kumtangaza mumeo. But before that be careful Maana mkiachana watu wanakuwa wana vitu vya kuku sema.Don't succumb to the pressure ya kushindanishwa na ex wako. Yani watu wanawafanya Kama wajinga, wanawashindanisha daily waone mtaishia wapi Na nyie mnawapa faida.All those videos ulikuwa unaweka snap chat of you and Idriss baadae zitakuja kukuhaunt, there is no need. Usishindane nao. Acha waweke video zao za kihindi and so forth wewe keep your love life private , utaona faida yake baadae. Acha waje kushtukia Wema anaolewa na mimba ya miezi 9 juu Wabaki wametoa macho. Au washtukie umeshazaaa kabisa waseme umeiba mtoto

Please achana na hawa marafiki Wema. Kama iki work out with Idris good for you, if not nakushauri tafuta mwanaume ambae hayuko hata Instagram au social media plssss ili akuongoze vizuri. Find a guy mwenye Maisha tofauti kabisa na ya kwako. Mkaka flani meneja wa benki Huyo ndo atakubadilisha completely but these guys wa kwenye mitandao Kama wewe issue itakuwa pale pale. Like ungekuwa Na mkaka wa benki huko kwanza hata Ile interview ya clouds angekukimbizaaaa angekuchapa vibao kabla hata hujatangaza hiyo mimba

WEMA SEPETU NA IDRIS SULTAN WAJA NA MPYA YA MWAKA...

Idris Sultan na mpenzi wake Wema Sepetu wanakuja na reality TV show ambayo itakuwa inazungumzia maisha yao.
Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Idris alisema ameamua kuungana na mpenzi wake Wema ili kuandaa project mbalimbali ambazo zitakuwa zinawaingizia pesa.

“Unajua mkiwa katika mahusiano halafu wote ni celebrity lazima angalau mfanye kazi mbili tatu ambazo zitawaingizia pesa,” alisema Idris.

“Zipo project nyingi lakini tunaanza na reality show. Hii ni nyingine na mpya na itakuwa inazungumzia matukio mbalimbali ya maisha yetu,” aliongeza Idris

Source:Bongo5

MIMBA YA WEMA YAZUA MAPYA.... IDRISS SULTAN APACHIKWA JINA LA DOKTA MWAKA BAADA YA WENGI KUSHINDWA KUMPA UJAUZITO WEMA


MIMBA ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu inazidi kuzua ya kuzua kila kukicha baada ya hivi karibuni, Mshindi wa Big Brother Africa Hot Shots 2015, Idriss Sultan ambaye anajigamba kuwa ndiye mwenye ujauzito huo kupachikwa jina la Dk. Mwaka.

Idriss amepewa jina hilo kwa vile Tabibu wa Tiba Mbadala Tanzania, Juma Mwaka Juma JJ Mwaka au ‘Dk. Mwaka’ amekuwa akisifika kwa kuwatibu wanawake wenye matatizo ya kutoshika mimba.

Mitandao mbalimbali ya kijamii wiki iliyopita ilimwita Idriss ni Dk. Mwaka huku ikimsifia kuwa, wameshindwa wanaume wengi, akiwemo Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliyewahi kuwa mpenzi wa Wema lakini yeye ameweza kumpa furaha mrembo huyo kwa kumpachika ujauzito.

“Kweli wewe Idriss ni Dk. Mwaka. Maana Mwaka amekuwa akiwasaidia wanawake kupata watoto. Wema ametoka na wanaume kibao, lakini wewe dogo umeweza, big up!” ulisomeka mtandao mmoja.
Gazeti hili lilimtafuta Dk. Mwaka kwa njia ya simu ili kumuuliza amelichukuliaje tukio la Idriss kuitwa kwa jina lake.

“Pengine uwezo wangu wa kazi umesababishwa aitwe hivyo. Lakini mimi bado nabaki kuwa Dk. Mwaka orijino na kazi yangu inajulikana,” alisema Dk. Mwaka.
Idriss hakupatikana hewani juzi kuzungumzia ishu hiyo lakini kwa nyakati tofauti amewahi kucheka tu kwa watu kumwita jina hilo.

MIMBA YA WEMA YAANZA KUONEKANA LIVE

MJENGO MPYA WA SUPER STAR WEMA SEPETU NI UTATA MTUPU


UTATA umegubika kuhusu umiliki wa mjengo aliohamia staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ambapo maswali yanayowasumbua wengi ni je, ameingia kwa kupanga au ameununua? Amani linakwenda sambamba na msomaji.

TUANZIE HAPA
Hivi karibuni, Wema aliyekuwa akiishi kwenye nyumba ya kupanga iliyopo Kijitonyama ya Makumbusho jijini Dar, alidaiwa kutimuliwa na mwenye nyumba baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco) kumtumbua jipu la madai ya kuchakachua huduma hizo.

Wema Isaac Sepetu
ATII AMRI, AHAMA
Wema aliihama nyumba hiyo usiku wa Ijumaa iliyopita lakini haikujulikana mara moja anakokwenda kuishi licha ya lori lililomhamisha, aina ya Toyota Canter kuandikwa nyuma, ‘Mtu Kwao’.

HABARI ZA JUMANNE SASA
Juzi Jumanne, chanzo kimoja kililipasha Amani kwamba Wema amehamia kwenye mjengo mkubwa na mzuri uliopo Ununio, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.“Jamani nilisoma habari kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda (ndugu na hili) la Jumatatu jana, zikisema kwamba Wema ametimuliwa kwenye ile nyumba ya Makumbusho lakini hamkusema amehamia wapi.
“Sasa mimi nawapa ubuyu. Wema amehamia hapa Ununio. Amepata nyumba nzima, kubwa. Lakini nisiwe msemaji wake mkuu, sijajua ni yake au amepanga,” kilisema chanzo hicho.
PAPARAZI WETU NYUMBANI KWA WEMA
Baada ya chanzo kuanika madai hayo, paparazi wetu alikanyaga mafuta akifuata maelezo ya chanzo mpaka kufanikiwa kufika kwenye nyumba hiyo.

SIFA ZA NYUMBA
Ni nyumba kubwa kuliko aliyokuwa akiishi Makumbusho. Ina eneo kubwa linalokaribiakaribia ukubwa wa uwanja wa mpira. Magari makubwa matano na madogo kumi yanaweza kuegeshwa eneo la wazi la ndani.
Pia Wema anaweza kufanyia ndani kwenye uwazi huo zile sherehe zake. Na kuna madai kwamba anaandaa sherehe kubwa kwa ajili ya kuumaliza mwaka 2015 akiwa mzima wa afya njema.
PAPARAZI AZUIWA KUINGIA NDANI
Hata hivyo, paparazi wetu alipotaka kufanya utalii wa ndani, alipigwa stop na msichana mmoja aliyejitambulisha kuwa ni ndugu wa Wema pia akimhoji paparazi wetu alifikaje ndani ya ukuta wa nyumba hiyo na kusema Wema hakuwepo.
Lakini kwa macho ya haraka, paparazi wetu alibaini kuwa nyumba hiyo ina vyumba vya kulala vinne, stoo, jiko, bafu na choo kwa ajili ya jumuiya, sehemu ya kulia chakula na sebule kubwa.
AMANI LAFANYIA KAZI UTATA
Licha ya msichana huyo kumkataza paparazi wetu kuzama ndani na kujionea kwa macho yake yaliyomo, alimuuliza kama anajua Wema ni mpangaji au mmliki. “Wema amejenga hii nyumba.
We huoni kuwa ni mpya! Watu wanadhani Wema hawezi kujenga nyumba siyo! Loo! Wataisoma namba mwaka huu,” alisema msichana huyo.
PETIT MAN
Katika kuchochea utata huo, paparazi wetu alibahatika kukutana uso kwa uso na mpambe mkubwa wa Wema, Petit Man ambaye jina lake halisi ni Ahmed Hasheem na kuzungumza naye kuhusu kutolewa Makumbusho na kuhamia huko kwa sasa.
Alisema: “Tena sasa tunahamia kwenye nyumba aliyonunua Wema mwenyewe. Bonge la nyumba, mtaipata habari yake. Iko Mbezi Beach.” (Ununio huhesabika kuwa ipo Mbezi Beach).
NANI MKWELI?
Madai ya msichana aliyekutwa nyumbani, anasema Wema amejenga nyumba hiyo. Ina maana alipata kiwanja, akatafuta mafundi, wakaanza ujenzi. Madai ya Petit Man ni kwamba Wema ameinunua! Kwamba, nyumba hiyo ilijengwa na mtu mwingine, akaamua kuiuza, akanunua Wema.
WEMA HAYUPO HEWANI
Juzi, paparazi wetu alimsaka Wema kwa simu ya mkononi ili kumsikia anasemaje lakini hakuwa akipatikana hewani.
MENEJA WA WEMA
Paparazi wetu alimpigia simu meneja wa Wema, Martin Kadinda na kumuuliza kuhusu umiliki au upangaji wa nyota huyo kwenye nyumba hiyo ya Ununio.
“Kusema kweli nilisafiri, ndiyo nimerudi usiku wa jana. Muda huu najiandaa kwenda kukutana naye. Nitakuwa na majibu baadaye,” alisema Kadinda.
Source:Global Publishers

IDRISS SULTAN KWA WEMA SEPETU KWISHA HABARI YAKE

Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo asubuhi, Idriss Sultan ameithibitishia dunia kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na staa wa movie Bongo Wema Sepetu na kwamba wanategemea kupata mtoto. 

Na haya ndiyo aliyoyaadika; "Me and You are not the ordinary. I sleep,eat, talk and wake up to only thinking about you. As much as utadhani kuwa you are blessed to have me no no i am blessed to have you. 

At 1st it was weird me kuangalia ndani ya kabati langu kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia vitu kama "Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike" au ukiingia jikoni kwangu and take over my house with good food. 

The way you look at other women wakinisogelea, how you always know when i need a kiss or a tight hug. The way you force me kuangalia Disney channel, how you wake up early these days to make me breakfast. I might bring you the most beautiful rose flower in the world and it will never look even half as beautiful as you are. When you're jealous unasonya sonya, when am jealous i smile. 

I would move mountains and planets just to make you happy. I will protect you, love you, spoil you, fight with you, cook with you, watch movies together, drive at night for no reason, sit with you and just stare at the stars. You're more than i ever asked for, you're my everything "My Wife"

Neno moja tu kwa wapenzi hawa
Rundugai Blog's photo.

Idriss Sultan Amtusi Diamond, Ajitapa Mtaani Kuwa yeye ni Kidume Aliyeweza Kumpa Mimba Wema

 
 Hii dharau! Siku chache baada ya staa wa Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kudaiwa kushika ujauzito ambao mhusika bado ni fumbo, balaa limezuka kufuatia Mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2015, Idris Sultan kudaiwa kumtusi zilipendwa wa mrembo huyo, Mbongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Risasi Jumamosi linakujuza.


TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Idris amekuwa akijitapa mitaani kuwa yeye ndiye kidume aliyeweza kumpa mimba Wema na kwamba ni daktari bingwa wa magonjwa sugu, yakiwemo ya uzazi kwani kwake kunapatikana tiba mbadala.


Majigambo hayo yanadaiwa kuharibu urafiki uliokuwepo baina ya wawili hao, kwani Diamond anachukulia kama ni kumtusi kwa vile aliwahi kujihusisha kimapenzi na Wema kwa muda mrefu bila kupata ujauzito.


KAMA KUNA URAFIKI NI KIINI MACHO
“Kitu ambacho watu hawaelewi ni kwamba hivi sasa urafiki wa Diamond na Idris ni kiini macho tu, kwani majivuno ya Idris ya kutoka na Wema yameleta uhasama mkubwa, hasa baada ya kujigamba kuwa ameweza kumpa ujauzito.


“Inadaiwa juzikati Idris akiwa na Wema sehemu, rafiki zake wakawa wanampongeza kwa taarifa zilizosambaa kuwa yeye ndiyo amemdunga mimba mrembo huyo ambapo kijana huyo alisikika akisema hakuna mwanamke asiyezaa duniani, isipokuwa kinachotokea ni kuto-match (kuendana) kwa damu za wawili. Eti kwa kitendo hicho yeye ndiye kidume cha mbegu,” kilisema chanzo hicho.


OMMY DIMPOZ NAYE ATAJWA
Ommy Dimpoz ambaye ni rafiki wa karibu wa Diamond, naye anatajwa kuwemo katika watu wanaompiga vijembe kwa kufurahia kitendo cha Idris kumjaza mimba Wema kwa kile kinachosemwa kuwa wawili hao wana ka-bifu ka chini kwa chini, kisa kikiwa siri yao.


“Ommy Dimpoz naye ni miongoni mwa watu wanaosapoti kwa asilimia kubwa Idris kumpachika mimba Wema na kwamba anaonesha wazi kuunga mkono kila kitu kinachofanywa na kijana huyo katika kumuumiza Diamond kupitia mimba hiyo.”


DIAMOND ANASA UBUYU
Habari zinasema kuwa maneno yaliyokuwa yakitembea katika kundi la Idris yalimfikia staa huyo wa muziki wa kizazi kipya nchini, ambaye alisikitishwa na kitendo cha kuonekana kama hakuwa na uwezo wa kumpa mimba Wema, akitamka kuwa wanaomsema hivyo hawajui jinsi yeye na Wema walivyokuwa wakiishi kimapenzi.


IDRIS HUYU HAPA, MSIKIE
Baada ya kumegewa ubuyu huo, juzi paparazi wetu alimtafuta mshindi huyo wa BBA aliyejishindia dola 300,000 (zaidi ya shilingi milioni 500) na kubahatika kukutana naye ana kwa ana katika eneo moja, nje kidogo ya jiji.


Alipoulizwa kuhusu ukweli wa madai ya kumtusi rafiki yake huyo, huku akichekacheka, Idris alishindwa kufunguka moja kwa moja, badala yake akasema hategemei kuja kuwa na tatizo na Diamond kwa sababu ya ujauzito wa Wema, hasa kwa kuwa tayari ana mtoto (Tiffah) aliyempata kwa mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari’.


“Diamond hawezi kuwa na mawazo hayo kwani haoni tatizo lolote kwangu kuwa karibu na Wema, hata nikizaa naye, kwa sababu uhusiano wao ulishamalizika.


“Hata hivyo hayo yatabaki kama madai. Mimi kuitwa kidume itatokana na namna waitaji watakavyokuwa wamenichukulia. Ila kiukweli sidhani kama kuna mtu anaweza kuja kuninunia kisa Wema maana suala la uhusiano au kuwa karibu na mtu inategemea tu na watu wenyewe jinsi wanavyoweza kuchukuliana na kuwaziana.”


KUANIKA KUHUSU MIMBA YA WEMA
“Suala la mimba ya Wema nitakuja kuliweka vizuri baada ya mwezi mmoja. Kwa sasa niache kwanza maana nina mambo mengi ya kufanyia kazi, sitaki kabisa kuanza kuvuruga mudi za watu na ndiyo maana naona hakuna haja kwa muda huu kuongelea ishu hiyo ila yasemwayo yanaweza kuwa na maana kama yameelezewa vizuri,” 


DIAMOND NAYE HUYU HAPA
Gazeti hili lilifanikiwa pia kumnasa mkali wa kibao cha Utanipenda? Diamond ambaye baada ya kuelezwa kilichopo alisema kwa sasa hana muda wa kusikiliza maneno ya watu wala kujibu kila anachosikia, zaidi anahangaikia maisha yake ili kuweza kufikia ndoto alizojipangia kwa vile maneno yapo kila siku na hayaepukiki.


“Dah! Mimi sioni kama kuna kitu cha ajabu wala kuzungumzia hapo, zaidi naweza kusema mimi sina muda tena wa kuanza kuzungumzia mtu ila kila mmoja atabeba mzigo wake.


“Kwa sasa nawaza kukuza muziki wangu kwa namna moja au nyingine, siwezi kuendelea kuwawazia watu wakati mwenyewe nina mambo mengi ya kujiwazia,” alisema Diamond.

Source:Global Publishers
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top