Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

TURUDI KWENYE MAMBO YA MSINGI


Nilisikitika sana kuona Rais mstaafu JK akiagiza Magari zaidi ya 700 kwa ajili ya Polisi.

Kinachonisikitisha na kunishangaza ni kwamba je tulikuwa na haja ya kuagiza magari mengi namna hiyo?

Turudi kwenye uhalisia wa mambo ya msingi.

Ukienda kwenye Hospitali za Serikali, Hakuna madawa, Mashine za CT scan zimeharibika wakati huo huo wagonjwa wakilala chini kwa kukosa vitanda.

Wanafunzi wa vyuo vikuu wanakosa mikopo na kukosa haki za kupata elimu.

Sasa nauliza je kulikuwa na umuhimu gani wa kuagiza magari kama hayo wakati kuna mambo mengi yanaharibika kwa fedha kukosekana?.

Wamachinga Ubungo wahamia Upande wa Pili wa Daraja Kuelekea Riverside

Kabla yakuvuka Daraja unakutana na viatu hapo chaguo ni lako Wewe unapenda kipi hapo ?
Hapo ni Ubungo baada ya Machinga kufukuzwa sasa wamehamia upande wa kulekea Riverside Barabara ya Mandela .
Ni Juu ya daraja unapata chungwa au kipande cha tikiti unapita zako hiyo ni Ubungo Barabara ya Mandela darajani ukielekea Riverside.
Daraja hilo limeshageuzwa kijiwe kama walivyokutwa hapo na kamera yetu wafanyabiashara hao wakipiga stori huku wakiendelea na kazi
Hapo darajani kazi zikiendelea bila wasiwasi hapo wanadai Mgambo hawafiki hivyo ni eneo huru kwao kufanya biashara muda wowote hayo ni madai ya Wafanyabiashara hao.
Biashara hapo ni za kila aina kama uonavyo Wauza dawa za kienyeji jamii ya kimasai wakiendelea na shughuli kama kawaida hapo wakitoa maelezo ya dawa kwa wateja waliokutwa hapo japo majina yao hayakufahamika mara moja.
Hapo ni pembeni ya Kituo cha Daladala kuelekea Buguruni kilichopo pembeni ya Barabara ya Mandela baada ya Kuvuka daraja pakiwa na wafanyabiashara ambao mwanzoni walikuwa pembeni ya SONGAS Plant.

Ujenzi wa Miundombinu ya Magari yaendayo kasi Katika Taswira.


Ujenzi wa Magari yaendayo kasi ukiwa katika awamu ya kwanza ya mradi ni eneo la manzese


NI kituo cha mafuta eneo la Manzese Darajani hapo




Kifusi kikubwa cha Mchanga pembezoni mwa Morogoro road eneo la njia panda ya mabibo ikionyesha kuwa kazi bado inaendelea maneo hayo.







Taswira zikionyesha maeneo katika Barabara ya Morogoro ambapo ujenzi unaendelea wa MiundoMbinu ya Magari yaendayo kasi wakiwa wameshatengeneza pembeni mwa barabara njia ambayo wanaishindilia mchanga.

Manzese Jana Jioni Machinga kama kawa









Kufuatia ujenzi wa miundo mbinu ya magari yaendayo kasi kuendelea Maeneo hayo ya Manzese kama uonavyo kwenye picha Machinga wamekuwa wakiendelea na kazi kama kawaida pale mafundi wanapoondoka kama ionyeshavyo eneo hilo pamechimbwa mtaro mkubwa lakini wao wameamua kuingi ahumo humo na kufanya biashara zao bila shaka yeyote kama walivyokutwa jana na kamera yetu ya Kijiwe wakichapa kazi bila wasi.

Jana Jioni Maeneo nje ya Ubungo Plaza




Jengo la Ubongo Plaza likionekana vizuri na kupendeza ikiwa ni mojawapo ya majengo mazuri yaliyopo maeneo hayo.

Taswira ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Bungeni Dodoma


Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo(kulia) akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Hamad Rashid Mohamed (kushoto) jana katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma wakati alipowasili katika Ukumbi kwa ajili ya kufuatilia Bajeti ya Serikali ya 2012/13.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dodoma.

TASWIRA:Mjini Hapa Usiulize umelala wapi


Kwa unawaona wakiwa wamelala na Pembeni ni Birika Kubwa la Chai liko Jikoni lishatengwa chai hapo wakiamka mambo yote ni hapo chai kwanza.

Huku mwingine akiwa amelala Pembeni yake aliesimama anatayarisha Chai kwenye birika hilo kubwa la chuma Hapo ndio maskani kwao hulala hapo nje au ndani ya hicho kijumba hii ni tarehe Juni 07 muda wa asbuhi saa moja.

Kwa uzuri kabisa waonekana wakiwa kwaanza ndio kumekucha usingizi umekolea hapo hawana habari ukiisha hapo kama kawaida chai kwanza ndio kila mmoja aingie mtaani kuzisaka shilingi.
Taswira hii ilichukuliwa tarehe Juni 12 mida ya asubuhi.Haijajulikana muda wanao lala vijana hawa ambao hawapungui watano wanaotumia eneo hilo la bustani lililopo Kinondoni B karibu na Hotel Ya Chichi.

Taswira la Usafiri

Hapo ni mtu nyomi au mizigo nyomi ?
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top