Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

SHILOLE APATA PUMZIKO JIPYAA

Baada ya kile kinachoonekana Shilole amepata pumziko jipya baada ya kutemana na Nuhu Mzwanda, leo ameweka picha akiwa na jamaa huyo na kuuliza swali kwa wadau kama kuna mtu kaibiwa....

Ameandika hivi

Shilolekiuno
Kuiba Waume za watu sijazoea! Je kuna mtu kaibiwa???

Shilole na Nuhu Mziwanda Basi Tena..Walivyoringishiana Wachumba Mpya Siku ya Valentines Day..

Kama ulikuwa ni msiba wa ‘penzi’ basi arobaini imeisha na sasa maisha yanaendelea kwa wasanii wa Bongo fleva, Shilole na Nuh Mziwanda ambao uhusiano wao umekufa na kuzikwa kabisa.
Wiki chache baada ya couple ya ‘shiwanda’ kuvunjika, na juhudi za wadau mbalimbali kutaka kuwapatanisha kugonga mwamba (soma hapa), inavyoonekana Nuh na Shishi kila mmoja ameamua kuendelea na maisha yake kwa kufungua ukurasa mpya wa mapenzi tena kwa vitabu tofauti...

Siku ya Valentines Day Kwao ilikuwa mashindano kila mmoja akiwa busy kupost picha akiwa na au jipya....Tazama picha:
Upande wa Nuh Mziwanda naye ameanza kupost picha za msichana mwingine mrembo anayetumia jina la Erah Erah kwenye Instagram, ikiwa ni pamoja na picha walizopiga pamoja kama couple, na mrembo huyo kupost pia kwenye ukurasa wake.

NUHU MZIWANDA AFUNGUKA 'SHILOLE HAKUWA MKE MZURI KWANGU NDIO MAANA NIMEFUTA TATTOO YAKE

Msanii Nuh Mziwanda amefunguka baada ya kuachana na mwandani wake Shilole, na kusema kuwa Shilole hakuwa mtu mzuri kwake, ndiyo maana ameamua kufuta hata tatoo ya jina lake aliyoichora.
Nuh ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba wakati yupo kwenye mahusiano na Shilole alishindwa kuonesha undani wake, ambao amekuja kuujua baada ya kuachana na penzi kuisha.

“Baada ya mapenzi kuisha mi nimekuwa adui yake, amehack acount yangu ya instagram najaribu kuwacheki wa kurudisha acount yangu wanashindwa kunirudishia anabana kila sehemu, kuna vitu ananifanyia vidogo vidogo ambavyo nimefanya kugundua kuwa hakuwa mwanamke mzuri kwangu, alikuwa anashindwa kuonesha true colour yake nimekuja kuijua baada ya kuachana naye”, alisema Nuhu.

Pia Nuh Mziwanda amesema iwapo wangeachana kwa amani na Shilole asingelazimika kuifuta tatoo hiyo, kwani ni ukweli usiopingika kwamba amemsaidia katika maisha yake.

“Mi ningeiacha tatoo kama Shishi ningeachana nae poa, kila mtu na maisha yake fresh tukionana tunasalimiana hakuna noma, lakini mwenzangu kwenye interviews anasema, akiitwa kwenye interview anaongea hiki kwamba mimi sina kitu, sijui nashindwa kusurvive nakula magengeni, anaongea vitu vingi ambavyo anajaribu kutoa fan base yangu, angekuwa mtu mzuri baada ya kuachana naye tatoo ningeiacha kwa sababu ningejua bado kabaki kuwa rafiki yangu na ni mtu ambaye alinisaidia”, alisema Nuh.

Pamoja na hayo Nuh amesema yeye binafsi hana chuki na msanii huyo ambaye alikuwa naye kwenye mahusiano, na kwa sasa ana mahusiano mengine ambayo asingependa kuyaweka wazi.

Mimi sina ubaya na Shishi , sina ugomvi naye na wala sitaki kufikiria kuja kuwa na bifu naye, nipo kwenye mahusiano lakini siwezi kuweka wazi mahusiano kwenye mitandao ya kijamii, sababu ni mke wangu yuko kwenye moyo wangu, hayupo instagram wala kwenye mitandao ya kijamii”, alisema Nuh.

STAA NUH MZIWANDA AMTUPIA MANENO HAYA SHISHI BABY

SHILOLE367 (2)
STAA wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana amemwangukia kwa mara nyingine aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika wakati mgumu tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao kama ilivyokuwa zamani.
“Ndugu yangu nikikwambia kuwa, Nuh maji yamemfika shingoni basi huna haja ya kuuliza mara mbili namna yalivyomfika kwani, juzikati nilikuwa naongea na Shilole akalalamika kwamba, jamaa huyo ameanza tabia ya kumpigiapigia simu akimwomba warudiane jambo ambalo Shilole analitolea nje,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, paparazi wetu alimtafuta Shilole kwa nia njema ya kutaka kujua ukweli wa madai hayo ambapo alisema ishu hiyo ipo ila hawezi kuanika wazi.
“Suala la Nuh kwa sasa sitaki kuendelea kuongea kwani nitakuwa nampigia debe mtu na kazi hiyo niliifanya sana. Unachotakiwa kujua kutoka kwangu ni kwamba mimi naendelea kupigania maisha tu ili niweze kusonga mbele na hapa nipo kipesa zaidi hivyo sina tena muda wa kuendelea kumpa nafasi bwana wa aina yeyote kwani hapo nyuma maisha yangu yalirudi nyuma hatua nyingi sana,” alisema Shilole.STAA wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana amemwangukia kwa mara nyingine aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika wakati mgumu tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao kama ilivyokuwa zamani.
“Ndugu yangu nikikwambia kuwa, Nuh maji yamemfika shingoni basi huna haja ya kuuliza mara mbili namna yalivyomfika kwani, juzikati nilikuwa naongea na Shilole akalalamika kwamba, jamaa huyo ameanza tabia ya kumpigiapigia simu akimwomba warudiane jambo ambalo Shilole analitolea nje,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, paparazi wetu alimtafuta Shilole kwa nia njema ya kutaka kujua ukweli wa madai hayo ambapo alisema ishu hiyo ipo ila hawezi kuanika wazi.
“Suala la Nuh kwa sasa sitaki kuendelea kuongea kwani nitakuwa nampigia debe mtu na kazi hiyo niliifanya sana.
Unachotakiwa kujua kutoka kwangu ni kwamba mimi naendelea kupigania maisha tu ili niweze kusonga mbele na hapa nipo kipesa zaidi hivyo sina tena muda wa kuendelea kumpa nafasi bwana wa aina yeyote kwani hapo nyuma maisha yangu yalirudi nyuma hatua nyingi sana,” alisema Shilole.
Chanzo:GPL

SHILOLE AKANA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA NJE YA NCHI LAKINI AKIRI KUSHAWISHIWA

Shilole amekanusha kujihusisha na kusafirisha madawa ya kulevya katika safari zake za nje lakini amekiri kuwahi kushawishiwa kufanya hivyo.

Muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV kuwa alikataa mtego huo kwakuwa hakupenda kuhatarisha maisha yake.

“Kiukweli ushawishi upo niache kusema uongo lakini kwa sababu binafsi na akili zangu timamu na najua nini nafanya basi huwa naweka tamaa pembeni na kuangalia kitu ambacho kina mwendelezo na maisha yangu,” alisema.

“Nikiwaangalia watu halafu nikiangalia mpenzi wangu ninavyompenda nimwache hivi hivi, roho inauma pamoja na watoto wangu, nawapenda sana. Halafu wananipa matumaini kwa sababu wana akili sana shuleni,”
alisisitiza.
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top