Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Wenyewe wako Kazini Mtaa Wa Kongo


Hapo Kila kitu ni 2500/= wanunuzi wakikaribishwa kwa kuonyeshwa magauni kwa kina Mama hiyo ndio Kongo wenyewe wakiwa kazini ambapo mtaa huo hufurika sana wachuuzi mbailmbali na wapita njia kuwa na wakatimgumu kupita mtaa huo.

Bling Bling hizo zikiwa zimepangwa kwenye meza hapo Mtaa wa Kongo

Biashara kila pembe hapo ni karibu na kituo cha daladala ziendazo Mnazi Mmoja Hiyo ni Kongo na wenyewe wakiwepo kama uonavyo ambapo mpita njia yeyote hupita kwa tahadhari kubwa kutokana na mbanano uliopo hapo.

Keraha za Mvua Tabata ''Tusiime''


Eneo hili liko usoni mwa shule Maarufu ya Tusiime Secondary na Msingi pia ambapo mara inyeshapo mvua eneo hilo huwa kero isiyoisha ya madimbwi makubwa ya maji hiyo ni kwa wapita njia hata magari ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo.

Kijichaka hicho kikionekana kustawi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.Hapo unaona dimbwi hilo likiweka eneo hilo kutopitika vizuri .

Gari ikitoka kuogelea kwenye dimbwi ambalo ni la tope

Taswira hiyo unaliona dimbwi mojawapo katika eneo hilo la Tusiime njia hiyo iko chini ya nguzo za kupitisha umeme mkubwa hivyo wananchi eneo hilo kushindwa kujua mwenye mamlaka ya kukarabati eneo hilo ili kuondoa maji hayo yasiwe yanatuamaa eneo hilo. Wengine wakienda mbali na kumtupia lawama mmiliki wa Shule ya kuwa kwanini hawaboreshei wateja wake eneo hilo ili liwe la kuvutia zaidi na kuondoa kero hiyo kwa wateja wake ambao wengi wao ni wale wenye kumiliki magari.

Eva na Suzzy

Eva na Suzzy wakishoo love baada ya misa ya Jumapili KKKT huko Moshono, Arusha. Picha kwa hisani ya mdau toka pande hizo za A-Town

Unapoambiwa Bomoa Hapa !!

Akiwa ameshamaliza Jengo lake la biashara kama kitega uchumi chake anajikuta anaambiwa umejenga chini ya nyaya za TANESCO unatakiwa ubomoe. Unaweza ongea lugha zote siku hiyo hiyo imemkuta mkazi mmoja wa Tabata njia ya kwenda Mtaa wa Ugombolwa ambae aliamua kuwekeza pembeni ya nyumba yake kwa kujenga fremu za biashara.Lakini kipindi chote hicho cha ujenzi mamlaka zote zilikuwa kimya bila hata kumpa onyo lolote hadi alipokuta ukuta una maandishi makubwa bomoa hapa.
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top