Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA MHE. JOSEPH WARIOBA KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 19 JUNI, 2012

HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
MHE. JOSEPH WARIOBA KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA
HABARI TAREHE 19 JUNI, 2012 KATIKA UKUMBI WA
KARIMJEE, DAR ES SALAAM

Ndugu Wanahabari,
Nianze kwa kuwashukuru kwa kuitikia mwaliko wetu. Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilianza kazi mwanzoni mwa Mwezi Mei, 2012 na kipindi hiki tumekitumia kwa maandalizi na sasa tuko tayari kuanza awamu ya kwanza ya kazi yetu, yaani kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi. Baada ya hapo itafuata awamu ya pili ya kuandaa taarifa, mapendekezo na Rasimu ya Katiba Mpya. Baadaye Tume itakutana na Mabaraza ya Katiba na mwisho Rasimu ya Katiba itafikishwa kwenye Bunge Maalum.

Kabla ya kuanza mchakato wa kushauriana na wananchi, ikiwa ni pamoja na safari za mikoani, tumeona ni muhimu na busara kukutana na nyinyi kwanza. Vyombo vya habari ni wadau wakubwa katika mchakato huu. Tume inaamini kwamba vyombo vya habari vina nafasi kubwa sana katika kufanikisha mchakato mzima hasa katika kutangaza maoni ya wananchi ili, licha ya kukusanya maoni tu, mchakato uwasaidie wananchi kubadilishana mawazo kuhusu aina ya Taifa wanalolitaka na aina ya Katiba wanayoitaka.

Ndugu Wanahabari,
Pamoja nami leo Wajumbe wote wa Tume, ikiwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti - Jaji Augustino Ramadhani, Katibu na Naibu Katibu.
Jukumu tulilokabidhiwa ni kubwa na muhimu kwa Watanzania, hivyo basi matayarisho tuliyokuwa tunayafanya yalikuwa na lengo la kuhakikisha mchakato mzima unakwenda kama ilivyokusudiwa.

Katika maandalizi yetu, tulitambua umuhimu wa elimu kwa umma kuhusu mambo yatakayozingatiwa katika Katiba. Ni wazi kuwa wananchi hawawezi kutoa maoni yao kwa ukamilifu bila ya kuwa na elimu ya kutosha. Kwa hiyo, kwa kuzingatia umuhimu huo, Tume imetumia muda mwingi kupata na kuandaa nyaraka muhimu kwa ajili ya kuwapatia wananchi elimu ya kutosha.

Tume imepata nakala elfu mia tano za Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977, nakala elfu kumi za Katiba ya Zanzibar ya 1984 na nakala elfu mia tano za Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83. Kwa kutambua kwamba nyaraka hizi hazitoshi, na hata kama zikipatikana kwa wingi ni vigumu kwa wananchi kuzisoma na kuzielewa kwa urahisi, Tume imeandaa nyaraka ambazo ni rahisi kuzisoma na kuzielewa.
Nyaraka hizo ni Katiba ya Jamhuri ya 1977, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, kwa lugha nyepesi, Hadidu za Rejea, Program ya Elimu kwa Umma na Utekelezaji wa Kazi za Tume. Nyaraka hizi tumeanza kuzisambaza na leo, tunawakabidhi nyinyi nyaraka zote ili msaidie kuzitangaza na kuelemisha wananchi. Aidha, Tume imeandaa vipeperushi kuhusu kazi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara.

Ndugu Wanahabari,
Hivi karibuni Tume itaanza safari za mikoani. Tume imejigawa katika makundi saba na kila kundi litafanya safari nne mikoani kati ya sasa na mwisho wa mwaka. Kila kundi litafanya kazi katika mkoa kwa wastani wa mwezi mmoja isipokuwa kwenye mikoa iliyo midogo kwa eneo, ambapo Tume itatumia muda mfupi. Tutaanza na mikoa minane ambayo ni Dodoma, Kagera, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Manyara, Pwani, Shinyanga na Tanga.

Tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi na kutoa maoni yao kwa uhuru, uwazi, bila ya hofu yoyote na kwa utulivu. Tunaomba wananchi wawe wavumilivu na watoe maoni bila jazba au kubeza. Tunaomba wananchi wawe wavumilivu sana kusikiliza mawazo ya wengine hata kama hawakubaliani na mawazo hayo.
Lengo letu kama Tume, ni kuhakikisha kuwa Watanzania kwa jumla wanatoa maoni yao. Tungependa sana kama ingeliwezekana, kila Mtanzania apate fursa ya kutoa maoni yake. Lakini, ukizingatia ukubwa wa nchi yetu na mazingira halisi, ni wazi haitawezekana kuonana na kila mtu. Pamoja na hivyo, ni kusudio letu kufanya kila linalowezekana kupata mawazo ambayo yataonyesha matakwa, mategemeo na mahitaji ya Watanzania wote. Katika upeo huo, basi tutafanya kila jitihada kwa njia mbali mbali kujaribu kuhakikisha kwamba maoni ya Watanzania kwa ujumla yanawasilishwa na kufanyiwa kazi vilivyo.

Pamoja na mikutano mbali mbali itakayofanyika katika mikoa yote, tutakuwa na mfumo wa kupokea maoni ya Watanzania wa kutoka pande zote za ndani ya nchi na nje ya nchi kupitia simu, barua pepe, mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na blogu na tovuti na pia kwa njia ya posta. Tunaomba wananchi wajitahidi kutoa hoja badala ya malalamiko peke yake. Mapendekezo ya mambo ya kuingia kwenye Katiba yatasaidia sana badala ya malalamiko tu.

Tume, kwa kiwango fulani imeanza kuratibu maoni ya wananchi yanayotolewa kwa njia mbali mbali. Mwelekeo wa kubaini maeneo ya kufanyia kazi unaanza kuonekana, hasa kuhusu taasisi za dola kama vile Serikali na vyombo vyake vyote na madaraka ya viongozi na taasisi mbali mbali. Tume inaomba maeneo mengine muhimu nayo yapewe uzito, hasa maeneo yaliyo katika Sura ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Sehemu hiyo ndiyo moyo wa Katiba. Yapo maeneo manne muhimu ambayo Tume ingependa kupata maoni ya wananchi.
Eneo la Kwanza, linahusu misingi ya Taifa. Misingi ndiyo nguzo ya utamaduni wa nchi na wananchi wake; misingi ndiyo nguzo ya nidhamu ya nchi na wananchi wake; misingi ndiyo nguzo ya maadili ya nchi na wananchi wake. Katiba yetu imetaja misingi mikuu kuwa ni uhuru, haki, udugu, amani, demokrasia na Serikali kutofungamana na dini yoyote ingawa wananchi wana uhuru wa kuabudu. Misingi hii ndiyo nguzo ya mshikamano na utulivu wa wananchi. Baadhi ya watu wanasema ama misingi hii haitoshi au imetelekezwa. Wengine wanasema inatosha. Tume ingependa kupata maoni ya wananchi kuhusu eneo hili.

Eneo la Pili, ni kuhusu mamlaka ya wananchi. Katiba ya sasa inaeleza kwamba wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na msukumo mkubwa wa mchakato huu wa kupata Katiba Mpya ni matakwa ya kuwawezesha wananchi kutunga Katiba yao. Lakini kuna watu wanasema mamlaka ya wananchi hayakufafanuliwa, wanasema mamlaka ya taasisi za dola kama vile Serikali, Bunge, Mahakama, Tume mbali mbali za kikatiba, na hata Vyama vya Siasa, yamefafanuliwa. Lakini mamlaka ya wananchi hayakufafanuliwa na wala hakuna utaratibu wa kuyatumia madaraka hayo. Wanasema wananchi wanatumiwa tu kisiasa wakati mamlaka yao yote yameporwa. Wengine wanasema mamlaka hayo yapo isipokuwa wananchi wameyakasimu kwa taasisi mbali mbali. Tume ingependa kupata maoni ya wananchi kuhusu eneo hili.

Eneo la Tatu, ni malengo muhimu na misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali. Malengo hayo yameelezwa vizuri sana katika Ibara ya 9 ya Katiba. Baadhi yake ni:-
•Kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;
•Kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;
•Kwamba mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi;
•Kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini.
•Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada za kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;
•Kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi.
Malengo haya ndiyo ndoto (vision) ya wananchi. Malengo haya ndiyo yanajumuisha matumaini ya Watanzania kuhusu aina ya Tanzania wanayoitaka. Mgawanyo wa madaraka kwa mamlaka mbali mbali za dola unakusudiwa kuhakikisha kwamba malengo haya yanafikiwa.

Baadhi ya watu wanasema kuwa malengo haya yanatosha ila hayatekelezwi kwa ukamilifu. Wengine wanasema kuwa hayatoshi katika zama hizi. Tume ingependa kupata maoni ya wananchi kuhusu malengo muhimu ya Taifa. Tume itapenda kufahamu ndoto za wananchi kuhusu rasilimali za Taifa na jinsi ya kuzilinda, kuziendeleza na kuzitumia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Tume ingependa kusikia ndoto za wakulima, wafanyakazi, wafugaji, wavuvi, wafanya biashara wakubwa na wadogo, wanaume, wanawake, wazee, vijana, walemavu na kadhalika.

Eneo la Nne, ni haki za binadamu na wajibu kwa jamii. Sehemu ya Tatu ya Sura ya Kwanza ya Katiba ina orodha ndefu ya haki na wajibu muhimu kwa raia. Baadhi ya watu wanasema haki hizi hazitoshi. Wengine wanasema haki za mtu binafsi zinadhulumu haki za jamii na wengine wanasema haki za binadamu zinaminywa au hazitekelezwi kwa ukamilifu au zinavunjwa. Tume inapenda kupata maoni ya wananchi.

Ndugu Wanahabari,
Awamu ya Pili ya uratibu na ukusanyaji wa maoni ya wananchi itafanyika kupitia Mabaraza ya Katiba. Wakati huo, Tume itawaomba wananchi watoe maoni yao kuhusu Rasimu ya Katiba. Kupitia kwenu, naomba wananchi kufika kwa wingi katika mikutano ya ukusanyaji wa maoni katika awamu zote mbili. Nawaomba wananchi kutoa mawazo yao kwa uwazi na bila ya hofu yoyote. Tume itafanya kazi zake kwa uhuru, uwazi na tunawahakikishia kwamba maoni yote yatakayotolewa na wananchi, taasisi, asasi za kiraia na makundi mengine yote yataheshimiwa na kufanyiwa kazi ipasavyo.

Ndugu Wanahabari,
Nimalizie kwa kurudia tena kwamba jukumu la vyombo vya habari ni kubwa katika kufanikisha kupatikana kwa Katiba Mpya. Pamoja na mambo mengine, wananchi wa sehemu moja ya nchi watafahamu maoni ya wenzao katika sehemu nyingine ya nchi. Naomba mlikubali jukumu hili ili kusaidia nchi ipate Katiba Mpya iliyo nzuri.
Nawashukuru.

MWANANCHI TOA MAONI JUU YA HOTUBA HII!

Mnyika:Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu!



Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu!

Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

Nape Nnauye afunguka baada ya Kauli ya Mh.John Mnyika ni Kupitia Ukurasa wake wa Facebook



Siamini kuwa watu wanajazba sana.,kwa kuwa najiuliza jazba yao inatokana na nini..? na sioni sababu iliyo dhahiri.,bali naamini ni mpango wa maksudi unaolenga kuzorotesha shughuli za bunge na kuacha kujadili yale ya msingi kwa kudeflect ajenda ya bajeti kuwa ni kampeni za kukipamba chama fulani na kukidharau na kudunisha chama kingine.

Ni ipi hoja Bajeti..? ama udhaifu wa Rais, au upuuzi wa CCM kama mnyika anavyodai..? Maneno haya ni ya kuudhi yanalenga kuamsha hisia za ukali na jazba ya watu ili wajibu hayo na kuacha mjadala wa msingi. Ni namna ya ku-sabotage
utendaji wa serikali na mhimili yake ikiwemo bunge..,ikiwa kazi ya bunge kwa mujibu wa katiba ni kuisimamia serikali na kuishauri..,siioni kazi hii ikifanyika ipasavyo bali naona kuwa bungeni kumegeuka kuwa uwanja wa kampeni na malalamiko..,

Niliwahi kusema hapo mwanzo kuwa wabunge waache kulalamika na watumie fursa ya bunge katika kushauri, kukosoa na kuirekebisha serikali na kuisimamia.

Mnyika amepotoka na analenga kupotosha wengine.,ni vema akijirekebisha na kutenda si kwa mihemko na hisia bali kwa uhalisia na uzalendo.

Mh.John Mnyika atolewa nje ya Bunge baada ya kukataa kufuta Kauli Yake



Tupo hapa tulipofikia
kutokana na Udhaifu wa Raisi,Bunge
legelege na Upuuzi wa CCM - John John Mnyika
Baada ya Kauli hiyo Naibu Spika Ndugai akamtaka afute kauli yake nae akasimamia kauli yake kwa kukataa kuifuta hivyo Naibu Spika kuamua kumtoa nje ya ukumbi wa Bunge kwa mujibu wa kanuni ya 73 a na bndizo zilizotumika.

Nape Nnauye akiwa Soko Kuu Iringa Mjini


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia Mkutano wa Hadhara Soko Kuu Mjini Iringa.

Nape na Oil Chafu


CHADEMA WAELEWA SASA MADHARA YA OIL CHAFU

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), kimetangaza rasmi kusitisha
kuwapokea viongozi wa ngazi zote
watakaohama kutoka Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na vyama vingine, baada ya kutemwa
katika kura za maoni kwa lengo la kutaka
kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama
hicho.
Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman
Mbowe, alitoa msimamo huo jana alipokutana
na wanafunzi wa vyuo vikuu vitatu vya Udom,
CBE na St John, katika hafla ya kuwaaga wenzao
wanaomaliza masomo yao.
Mbowe alisema kuwa, CHADEMA kinataka sasa
kupata viongozi na wanachama wanaosukumwa
na uzalendo wa kweli, na wanaoamini itikadi na
sera zake, na si wanaotaka kukitumia kama
ngazi ya kufanikisha malengo yao.
Alisema wamejifunza kwa kiasi kikubwa hasara
ya kuwapokea wanachama, na hasa waliokuwa
viongozi wa vyama vingine dakika za mwisho,
hususan wakati wa uchaguzi, hivyo kuanzia sasa
hawapo tayari kufanya hivyo.
Mbowe alisema wapo tayari na
wanawakaribisha wanachama ama viongozi wa
CCM ambao wanaona kuwa CHADEMA ni chama
makini, kikomavu na wanaoamini kina malengo
halisi ya kuikomboa nchi na kuwaletea
maendeleo wananchi wote bila kujali itikadi ya
vyama, dini, kabila ama eneo la nchi.
“Wale wapambanaji waliochoshwa na matendo
ya wenzao ndani ya CCM, na wanaoamini kwa
dhati kabisa na kusukumwa na dhamiri ya kweli
ya kupigania maslahi ya wanyonge, waje sasa.
“Hakuna haja ya wao kusubiri hadi dakika za
mwisho, na hasa pale wanapopigwa chini katika
kura za maoni ndio waje. Wajue kuwa
wakisubiri muda huo, hawataweza kupokelewa
hata kama watakuwa ni wazuri namna gani,”
alisema Mbowe.

BAVICHA yawageukia wasomi


na Abdallah Khamis
BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limewataka wasomi nchini kutambua wajibu wao wa kulitumikia taifa, ikiwa ni pamoja na kusimamia misingi iliyoachwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika kuleta maendeleo ya nchi.

Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche, alitoa kauli hiyo jana alipowahutubia wanachama wa chama hicho kutoka vyuo vya CBE na DIT katika sherehe maalumu ya kufungua matawi ya CHADEMA katika vyuo hivyo, iliyofanyika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.

Alisema wasomi wengi wakiwa vyuoni mawazo yao yanalenga kuingia ofisini na kuwa na nyumba bora za kuishi, bila kuwafikiria Watanzania wanaotaabika katika lindi la umaskini, huku nchi ikiwa na rasilimali za kutosha.

“Miaka miwili iliyopita nilikuwa kama ninyi katika harakati za vyuoni, ninachoweza kuwasihi ni kwamba muepuke kukariri yaliyoandikwa na wana-philosophia bila kufanyia kazi, kwa maana kama mtakuwa hamuwezi kuwasemea Watanzania, basi elimu yenu itakuwa haina manufaa yoyote,” alisema Heche.

Alisema ni aibu kwa wasomi wa Tanzania kufundishana namna ya kuomba fedha kupitia miradi mbalimbali wanayoandika na kuwatafuta wafadhili wa kuwapatia fedha, huku wakipishana na wafadhili hao wakiwa wamebeba rasilimali za Tanzania na kuzinufaisha nchi zao.Akizungumzia bajeti ya serikali iliyotangazwa hivi karibuni, Heche alisema ni aibu kwa nchi, kwa kuwa asilimia kubwa inategemea utashi wa wafadhili, na kwamba wakiamua kugoma kuisaidia nchi itakuwa imeshindwa kujiendesha.

Aliwasisitiza wanavyuo hao walioamua kuwa wanachama wa CHADEMA wasihofu kuingia katika ulingo wa kugombea nafasi za uongozi wa nchi kwa kile alichoeleza ukombozi wa kweli hauwezi kutoka kwa watu waliolelewa katika fikra za CCM.

Alisema mfumo mbaya wa uongozi ndiyo unaompa rais madaraka ya kufanya anavyojisikia, bila kujali hisia za wananchi na kutolea mfano uteuzi wa Diodarus Kamala, Philip Marmo na Batilda Burhani kuwa mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali, licha ya wananchi katika majimbo yao kuwakataa kuwa hawafai kuwaongoza.

Aliongeza kuwa, katika mfumo huo huo wa uongozi usiojali hisia za wananchi, ndipo wanapopatikana watoto ambao wazazi wao walikuwa katika nafasi za uongozi katika serikali na chama, na wao leo ni viongozi wa maeneo waliyaoacha wazazi wao.

“Mnawashuhudia leo kuna Nape Nauye, watoto wa mzee Kawawa na hata Adam Malima, leo ndiyo viongozi wetu kama Tanzania hakuna watu wengine wa kushika nafasi hizo,” alisema Heche.
Tanzania Daima

CHADEMA wafunika Iringa Leo





Mbunge wa Iringa Mjini Mh.Peter Msigwa akishirikiana na makamanda wengine alifanya mkutano wa hadhara leo katik Operation ya Vua Gamba Vaa Gwanda. Hiyo ni sehemu ya Umati uliohudhuria Mkutano huo

Slaa asema serikali imechoka


na Edson Kamukara
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameiponda hotuba ya bajeti iliyosomwa bungeni juzi, akisema inaonyesha wazi kuwa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imefikia mwisho wa kufikiri.

Alisema kuwa kitendo cha serikali kushindwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato na badala yake kuendelea kutegemea vinywaji laini na vileo na kuruhusu wananchi waweke majina yao kwenye pleti za magari badala ya namba za magari ni hatua kuwa hawana ubunifu wa kukuza uchumi.

Akizungumza na Tanzania Daima jana jioni kwa njia ya simu kuhusu bajeti hiyo, Dk. Slaa ambaye alikuwa mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, alisema licha ya kwamba ni mapema kutoa maoni lakini bajeti imejaa matamko ya kisiasa.

“Hayo aliyosoma Waziri William Mgimwa ni matamko ya kisiasa si hotuba ya bajeti, kwani tunaoelewa bajeti ni vitabu vinne wanavyopewa wabunge, nami navingojea nimeomba nipatiwe ila kama ndiyo hivyo alivyosoma tuko kwenye hali mbaya,” alisema Dk. Slaa.

Alisema kuwa kinachoshangaza ni kuongezeka kwa deni la taifa halafu fedha zinazokopwa na serikali imezielekeza kwenye matumizi ya kawaida badala ya maendeleo.

“Taifa linakopa ili iweje, kulipana mishahara na posho ama? Hii ni hatari kwa vizazi vijavyo miaka 30 hadi 40 ijayo. Zamani hata serikali zilizotangulia zilikopa lakini mikopo hiyo ilitumika kujenga viwanda, shule, barabara na huduma nyingine, leo tunafanya hivyo?” alhoji.

Alisema inashangaza kuona serikali inakopa kutoka vyombo vya biashara halafu inapelekea fedha hizo kwenye uendeshaji jambo lililozifanya hata taasisi za fedha za kimataifa kuwanyima mikopo na hivyo wamekimbilia kwenye mabenki.

Alifafanua kuwa ni katika makosa kama hayo imenyimwa mkpo wa sh bilioni 480 kwa ajili ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO).

Kuhusu vyanzo vya mapato, Dk. Slaa alisema anashangaa kuona kila mwaka serikali akili yake inalalia kuongeza kodi kwenye vileo na kuacha sekta nyeti kama madini.

“Tumerudia vyanzo vile vile ukiacha hicho cha watu kuruhusiwa kutumia magari yenye majina yao badala ya namba za usajili, sasa labda walevi watakapogoma kunywa ndipo serikali itapata ubunifu wa kuangalia vyanzo vingine,” alisema.

Hata hivyo, Dk. Slaa aliponda chanzo kipya cha mapato cha kuwaruhusu watu kuweka majina badala ya namba, akidai kuwa hatua hiyo mbali na kuleta matabaka kisaikolojia kwa wenye fedha kujiona wameiweka serikali mfukoni lakini pia ina madhara kuichumi.

“Mafisadi hawaoni uchungu hata kidogo kutumia fedha ila jambo la msingi ni kwamba wamezipataje, sasa kwa hali kama hii watafurahi kwa vile wanaona serikali imewahalalisha bila kujali kama fedha zao ni haramu,” alidai.

Aliongeza kuwa hata, vipaumbele ambavyo serikali imeelekeza kwenye bajeti yake, utekelezaji wake utakuwa mgumu kwani fedha zilizotengwa ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi.

Tanzania Daima.

Nape aendelea na Ziara yake Iringa







Taswira za Operation Vua Gamba Vaa Gwanda Uwanja wa mpira KIA Jumapili iliyopita.


Hao ndio Makamanda waliongoza operation Vua Gamba Vaa Gwanda iliyofanyika Uwanja wa Mpira KIA iliyoongozwa Na Kamanda Magoma Jr Magoma anaeonekana akisoma KAtiba hapo.

Kamanda Deborah(BAVICHA HAI) akihutubia katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mpira KIA.


Kamanda Magoma Jr Magoma akiwapongeza Makamanda walioandaa Mkutano huo wa hadhara hapo viwanja vya mpira KIA.




CHADEMA NI CHAMA CHA WAZALENDO NA WANYONGE WA TANZANIA, KAMANDA MAGOMA Jr AKIKUSANYA MICHANGO YA KUCHANGIA CHAMA KUTOKA KWA WAPENZI WA WACHAMA WA CHADEMA-KIA (OPERATION VUA GAMBA/ VAA GWANDA
(Picha na David Jr.Magoma-Arusha)







© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top