Loading...
Home » Posts filed under Daladala
Daladala Time:Leo tuko na Kondakta kama kawaida Swagazzz !!
Hapo gari limeondoka Konda hajampa pesa mpiga debe ikabidi tejaa adai chake kama hivyo uonavyo kampandia konda nae bila hiyana ikabidi ampe gawio lake
Kondakta wetu huyo leo ambae anahudumu daladala ya Mwenge-Kariakoo Japo suti yake ni safi tofauti na wengi wao ambao ni wachafu lakini bado uvaaji wao ni wa mashaka kama uonavyo huwa hawalipendi vazi hilo japo ni Lazima wavae unifomu wao wanakuja na swagazz zao .
Filed Under:
Daladala
on Monday, June 18, 2012
Daladala Time:Swaga za Kondakta Leo


Katika Daladala time leo tuko na Konda wetu ambae jina lake halikufahamika mara moja anahudumu katika daladala inayofanya kazi kati ya VINGUNGUTI na KAWE hiyo ndio vazi lake nguo juu ya nguo.
Chini hapo bila matatizo ameutilia kiatu hicho huyoo ndio konda wetu hana hiyana na mtu katulia tuli.
Filed Under:
Daladala
on
Usafiri unavyokuwa Kero Muda wa Jioni

Hapo ni Mtaa wa Kongo Taswira hii ya Saa Kumi Na MOja hii kila mmoja anataka wahi nyumbani akapumzike baada ya shughuli za siku nzima.Daladala hilo ni la Mnazi Mmoja kuelekea Tabata Segerea likiwa limezongwa na abiria kila mmoja akitaka awahi kiti akae apumzike kwani njiani huko hujui kama foleni itakuwaje pia na mchoko wa siku nzima unapelekea abiria hao kuwa na 'vita rafiki'maana baada ya kuingia ndani kinachofuata ni vicheko na maneno ya hapa na pale.Hapo lazima Lazima uende na daladala Mnazi kwa kulipia sh.200 ndio utoe Nauli ya Segerea Shs.400 Jumla Kuu unalipa sh.600/= ili ufike Tabata Segerea.
Kina Mamaa sasa Pochi Kwapani kama kawaida.
Filed Under:
Daladala
on Tuesday, June 12, 2012




