Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Neno La Leo kutoka kwa Mbunge wa Iringa Mjini


changamoto kubwa katika maisha ni kujua nini cha kufanya, tunaamka kila siku asubuhi kwa ajili ya shughuli za kila siku, je huwa tunafanya yale tuliyopaswa kufanya?kila siku tunajikuta tunapaswa kuamua kipi cha kufanya .with all the options and choices that lie before us every day. Hilo ni swali gumu. Je? Unajua nini cha kufanya na maisha yako? Kitu gani kinakusukuma kutoka kitandani kila asubuhi? Tafakari,.jiulize .have a great day.

Kutoka Facebook:Nape ana Neno kwa Waheshimiwa Wabunge


HIVI KWANINI WABUNGE WETU WANALALAMIKA JUU YA BAJETI BADALA YA KUTIMIZA WAJIBU WAO?! WANAMLALAMIKIA NANI? Kimsingi bajeti inapopelekwa Bungeni na serikali inakwenda kwa ajili ya mjadala na marekebisho palipo na mapungufu NA SI KUPITISHWA KAMA WAJIBU TU, tunategemea mjadala wenye lengo la kiboresha kwa faida ya wananchi. Sasa haya malalamiko ya baadhi ya wabunge barabarani, mara " niko tayari kufukuzwa"!! Nani anamfukuza nani?! Nani anayetishia uhuru, haki na wajibu wa kikatiba wa wabunge wetu mpaka wanalalamika barabarani?!! Nashauri wabunge timizeni wajibu wenu, jadilini na kuishauri serikali ndani ya bunge juu ya maboresho ya bajeti iliyoletwa kwenu!

Kwenye Facebook yake:Nape aeleza kuhusiana na yaliyojiri Bungeni Leo kuhusiana na Hali ya Uchumi




Nilikuwa nikisikiliza Bunge na kusikia hotuba juu ya hali ya uchumi hapa nchini na nikajiuliza hivi hawa "watani" wetu wanaopita kuchangisha watu nchi nzima na kunadi kuwa hali yetu ya kiuchumi ni "mbaya sana" na wengine wakaandika makala kwenye magazeti kuwa serikali haina hata uwezo wa kuagiza mahitaji ya mwezi nje ya nchi na HAZINA imekauka..,nilijiuliza kuwa hayo wameyatoa wapi..? ni uvivu wa kufuatilia na kusoma ripoti za serikali juu ya hali ya uchumi au ni dhamira ya kukusudia kupotosha na kudanganya umma wa watanzania..,

Nimekuwa nikisoma na kufuatilia ripoti na taarifa mbalimbali za uchumi za nchi mbalimbali duniani na kufarijika baada ya kugundua kuwa hali yetu ya kiuchumi inaelekea vizuri kuliko nchi nyingi hata zile zinazotajwa kuwa zilizoendelea za kule Ulaya na Asia.

Mathalani kwa India, takwimu za uchumi zinaonyesha kuwa GDP imeendelea kushuka kwa 5% tangu mwaka 2010.,according to economic watch.,Ugiriki wamekuwa wakitapatapa kujinasua kwenye madeni makubwa waliyonayo,lakini pia wanayo hatari kubwa katika kupungukiwa nishati ya umeme ambayo ni msingi katika shughuli za uzalishaji nchini humo hata serikali kulazimika kutumia dola milioni 50 za dharura kutoka hazina yao kukabiliana na hatari hiyo. Na hii ni nchi yenye watu wasiozidi milioni 11.5.

Pia, Benki ya dunia imeonesha wasiwasi wake juu ya hali ya ulaya kwa sasa na athari zitazopatikana katika uchumi wa dunia, hata kufikia Benki ya Dunia kushauri nchi za ulaya kuelekeza nguvu zaidi katika mipango na miradi yao ya muda mfupi na muda wa wastani na kuacha kufikiri na kupanga mipango ya kimaendeleo ya muda mrefu.

Nadhani watanzania sasa tunapaswa kuelekeza masikio yetu na macho yetu Dodoma ili kupata uhalisia wa hali yetu kiuchumi na namna tunavyoendelea kuimarika kiuchumi.

Nimefurahishwa na majibu ya waziri wa Nishati na Madini Mhe, Sospeter Muhongo pale aliposema kuwa sasa wanatekeleza mipango ambayo si tu itahakikisha Nishati ya umeme inapatikana Tanzania bali wana-projections kugeuza Tanzania kuwa ni wazalishaji-wauzaji wa Nishati hiyo, na hivyo wamelazimika kuanza kuchimba madini ya Uranium kabla ya Kenya.

Tuendelee kusikiliza Bunge letu litakaloendelea tena saa kumi Jioni.

Kutoka Facebook Kaka Mubelwa Bandio anasema..


MAPENZI ni kama MCHEZO ana VITA tuuuuu!!!
Yaani ...... Ili ushinde ni lazima ujue KUSHAMBULIA na pia KUZUIA.
Kama ambavyo huwezi shinda mechi ya soka wakati "ma-forward mbele wanakazana na mabeki nyuma wanaachia".....
Ama kama ambavyo huwezi kushinda vita kwa kujua kufyatua risasi ilhali hujui namna ya kujikinga na kujificha.....
Vivyo hivyo katika mahusiano huwezi kuendelea kuvutiwa nayo kama "kilichokuvutia kuwa na uliye naye hakitunzwi"
Kushinda jambo lolote si kazi kama kutunza ushindi huo.

Kama anakuvutia, basi jua kuwa ANAWAVUTIA, na namna UNAVYOMVUTIA, ujue kuwa unawavutia. Ni wewe wa kuTUNZA mvuto wake kwako (usinyakuliwe na wengine) lakini pia kuHESHIMU mvuto wako kwa wengine ili ubaki naye.

Kwani, wengine wanaongozwa na UTASHI na sio MAPENZI.

Nawaza kwa sauti tuuuuuuuuuu!!!!!!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top