WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
E Mungu twaomba uilinde
Jumuiya ya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu
Jumuiya yetu zote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu
Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu
Jumuiya yetu zote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu
Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora
Jumuiya yetu zote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana