Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Ukweli wa kaka’ke Diamond kubaka Sweden

rommy
Kaka wa staa wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Rommy Jones.

STORI: Musa Mateja, Wikienda
Dar es Salaam: Mwisho wa utata? Hatimaye ukweli juu ya sakata la kaka wa staa wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Rommy Jones umeanikwa ndani ya Ijumaa Wikienda ambalo ni namba moja kwa habari za mastaa ndani na nje ya Bongo.


Kabla ya gazeti hili kuchimba undani wa msala huo, kulienea tetesi mbalimbali kuwa Rommy ambaye ni DJ rasmi wa Diamond na mmoja wa wafanyakazi wa Wasafi Classic Baby (WCB) kuwa amebaka kisha kukimbia nchini humo bila kuelezwa undani wa tukio hilo.

WIKIENDA MZIGONI
Katika kusaka undani wa sakata hilo, wikiendi iliyopita Ijumaa Wikienda lililazimika kuzungumza kwa nusu saa na Meneja Matukio ya Kimataifa wa Diamond, Sallam Sharaff.

Akisimulia kilichotokea, Sallam alisema kuwa maneno yaliyozagaa mtaani na kwenye mitandao ya kijamii yalielemea kwenye ushabiki na hata yanavyoelezewa hakuna anayetambua undani wa tukio hilo lilivyojiri.

Sallam alisema, ukweli wa kila jambo wanafahamu zaidi familia ya Wasafi, hasa wote waliokuwepo kwenye Ziara ya Ulaya.

BOFYA HAPA KUMSIKIA SALLAM
“Mara kadhaa nimekuwa mzito sana kuongelea suala la Rommy Jones kufuatia baadhi ya watu kulichukulia tofauti kabisa na ilivyotokea.

“Ishu hiyo ni kweli ilitokea lakini ninachoweza kusema ni kwamba ulikuwa ni mchezo mchafu ambao ulilenga kuichafulia jina WCB.

“Madai ya Rommy Jones kubaka siyo ya kweli kwa sababu mimi ninachokijua ni kwamba, huyo mrembo aitwaye Debora alikuwa akiwasiliana na Rommy Jones siku kibao yaani ni zaidi ya miaka miwili huko nyuma.

diamond33Rommy akiwa na Diamond.

WATUA SWEDEN, DEBORA AJUA
“Siku tulipofika Sweden tu, Debora alijua kuwa Rommy Jones yupo ‘so’ alimnunulia zawadi ya simu na kumletea kwenye apartments (nyumba za kuishi) tulizokuwa tumefikia na jioni yake akamtumia gari, likaja kumchukua na kumpeleka kwake.

“Kusema kweli sisi huko nyumbani kwa Debora hatukupafahamu ila siku hiyo alimrejesha mapema, tena wakiwa na furaha ya hali ya juu.

“Sisi wote tukaanza kumtambua kama shemeji yetu hivyo jambo la kubakwa hapo sijui linatokea wapi…

“Ukiachilia mbali hiyo, siku iliyofuata mimi nilikuwa nimetoka, baada ya kurudi muda wa jioni sikumkuta Rommy Jones, nilipoulizia nikaambia Debora amemchukua na kuondoka naye.

“Alilala huko na kurudi asubuhi yake maana tulikuwa tunaenda kufanya shoo kwenye mji mwingine.

MCHEZO MCHAFU?
“Ujue ishu hii mimi baadaye nilikuja kugundua kwamba kuna namna ambayo Debora alikuwa akitengeneza mazingira ya kutafuta pesa kwani sheria ya Sweden siku zote ukilala na mwanamke bila ridhaa yake akishitaki unatuhumiwa kuwa umebaka na yeye analipwa kama dola elfu kumi na mbili (zaidi ya Sh. milioni 24 za Kitanzania).

HATA MKEO?
“Hata kama ni mkeo, ukifanya naye tendo la ndoa bila yeye kuridhia na akashitaki, basi wewe utakuwa umebaka na sheria inakufunga huku yeye akilipwa kiasi hicho cha fedha.

salam menejaMeneja wa Diamond, Sallam Sharaff.

KILICHOTOKEA SASA
“Kilichotokea kwa Rommy Jones ni dhahiri kabisa kuwa Debora alitaka kujipatia pesa kwa njia hiyo kwani baada ya kuanza kung’aka kuwa amebakwa, mimi nilimtafuta na kumuomba msamaha maana Rommy Jones hakujua kama sheria ya huko iko hivyo na isitoshe wote walikuwa wamelewa.

“Pamoja na msamaha, Debora aliendelea kuomba afidiwe dola elfu kumi na mbili, mimi nikamwambia nimpatie dola elfu sita lakini aligoma na kutaka hiyo hivyo tukashindwa kuafikiana.

VITISHO KWA DIAMOND
“Baada ya kuona tumeshindwa akaanza kututishia kuwa Diamond ni kaka yake hivyo anahusika na msala huo.

“Kweli polisi walifika na kumkamata Diamond, tukawaambia kuwa Rommy Jones si DJ wetu na kwamba tulimkodi tu na tayari ameshaondoka zake kwao.

“Baada ya kuona hivyo hawakuwa na jinsi, wakamwachia Diamond na sisi tukaendelea na shoo zetu.

“Hayo yote yalitokea tukiwa tumebakiza shoo mbili tumalize ziara hiyo hivyo Rommy Jones akawa ‘wanted’ ndiyo maana aliondoka mapema kurejea Tanzania,” alimaliza kusimulia Sallam.

DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Rommy Jones simu yake haikuwa hewani lakini kwa upande wake Diamond alisema kuwa Sallam ndiye mwenye mkanda mzima hivyo kama alishafafanua ndivyo ilivyokuwa.

TOUR YA DIOMOND UROPA YAZUA MENGI Dj Rommy Jones Kwenye Kashfa ya Ubakaji Sweden...


Inasmekana alimbaka mdada wakibongo aishie sweden anaitwa Deborah
Shutuma hizo zimewekwa Instagram katika page mbali mbali zinasema Rommy alikuwa na dada huyu nyumbani kwake na kumuwekea kilevi kwenye kinywaji chake akasinzia na jamaa kufanya yake...

Wadaku wanadai Rommy Jones hakumaliza ziara ya chibu chibude huko ulaya kwani alikimbia soo na chat sms zimewekwa hadharani akiomba msamaha
wambeya wanadai meneja wa diamond aitwaye salaam alikuwa radhi kutoa euro 10,000 ili kuua soo ila bidada akakataa....

Kwa Habari zaidi Ingia Page ya Dougie masta huko insta...
or Jamii Forums

HUYU NDIYE SUPER STAR DIAMOND PLATINUMS APATA SHAVU JINGINE LA NGUVU BAADA YA KUTOKA TOUR

Wanasema hela zinaenda kwa wale ambao tayari wanazo. Kwa Diamond kuamka na dili mpya kila kukicha kimekuwa ni kitu cha kawaida.
Na sasa staa huyo amesaini mkataba wa ubalozi wa tomato sauce tunayokutana nayo mara kibao kwenye vile vijiwe vya kulia viepe, Red Gold.
Amesaini mkataba huo jana kwenye ofisi zake za WCB. Huo ni mkataba wa tatu baada ya DSTV, Vodacom.

HIVI NDIVYO DIOMOND PLATINUMZ "BABA LATY" ALIVYOPOKELEWA TURKANA KENYA

Diamond Platinumz “Kwenye Mitaa!!!....Molah nakushkuru kwakuwa naamini hizi zote ni baraka zako.... ila tu niwakumbushe ndugu zangu kuwa "Kuku hata umlishe nini kamwe hawezi kunyonyesha!"..... NAIROBI get ready for your Platnumz!!! AMERICA | EUROPE see you soon!”

FAMILIA ya Mwanamuziki Diamond Platnumz ilivyotengeneza Mamilion ya Pesa Kutoka Vodacom YALAMBA MKWANJA WA MAANA

FAMILIA ya mkali wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ imelamba mamilioni ya shilingi kufuatia mkataba walioingia hivi majuzi na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom, Risasi Mchanganyiko lina ripoti kamili.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ya kampuni hiyo yenye mtandao mkubwa zaidi wa simu nchini, Diamond na familia yake inayowahusisha mama yake mzazi, mzazi mwenzake Zarinah Hassan na mtoto wao Tiffah, wamepewa kiasi cha shilingi milioni 700.

“Mimi nipo hapa, mkataba umefanywa kwa usiri mkubwa na unajua haya mambo yanakuwaga kisheria zaidi, lakini dogo (Diamond) kalamba siyo chini ya milioni 700, nadhani ndiyo msanii wa kwanza Bongo kupata mkwanja wa maana kwenye haya matangazo ya biashara,” kilisema chanzo hicho.

Wakati chanzo hicho kikitoa madai hayo, katika baadhi ya mitandao ya kijamii, kiasi cha fedha kinachotajwa kutolewa katika mkataba huo ni kiasi cha dola 650,000.
 
 
Gazeti hili lilimtafuta Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu ili azungumzie madai hayo ikiwemo kiasi halisi ambacho Diamond alipewa.

“Ni kweli kuwa ni jambo jema kama wasanii wachanga na wengine wakijua kiasi halisi cha fedha ambacho Diamond amepewa, ila suala hili lipo kisheria, nitakuwa nimevunja sheria endapo nitasema, kifupi ni kwamba amesaini mkataba mnono na kama Vodacom, tutaendelea kuwasapoti wasanii wetu wa ndani na maisha yao yataendelea kuwa murua.
 
 
“Tunachoomba ni kwa wasanii wetu kujituma zaidi na kuwa kioo cha jamii kwa kuwawakilisha Watanzania kwa uweledi,” alisema.

Alisema Vodacom imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Diamond, lakini milango ipo wazi kwake kuweza kusaini upya baada ya huu kumalizika. Aidha, alisema msanii huyo ndiye pekee aliyesainishwa na kampuni yao, lakini Aprili mwaka huu, ambao ni mwezi wa kuanza kwa bajeti yao mpya, wanategemea kuwasainisha wasanii zaidi wa Bongo Fleva.

Kwa upande wake, mmoja wa mameneja wa Diamond, Babu Tale, alikiri msanii wake kupata mkataba mnono kuliko aliowahi kupata msanii yeyote kabla, lakini hata hivyo hana mamlaka ya kutaja kiasi, kwani ni suala binafsi la Diamond.

“Kwanza nikusaidie, hakuna kampuni ya ndani hivi sasa inayoruhusiwa kutoa malipo kwa dola, fedha zote zinatolewa kwa shilingi, lakini kwamba ni kiasi gani kwa kweli siwezi kusema, ila mkataba wake ni mnono kuliko msanii yeyote Bongo kwa sasa.”

Juhudi za kumtafuta mkali huyo anayetamba barani Afrika kwa sasa zilishindikana kwani hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, taarifa zilisema alikuwa Afrika Kusini.

Chanzo:GPL

DIAMOND PLATNUMZ AFUNGUKA KUHUSU WIMBO WAKE MPYA ANAEUTOA IJUMAA HII...SOMA HAPA ALICHOSEMA


AFRICA!!!! i know you been waiting for this...and it's ready for You!... TANZANIA + SOUTH AFRICA = HIT..this Friday!

( kwanza kabisa ningependa kumshkuru Mwenyez Mungu kwa kuweza katusaidia kufanikisha ndoto zetu za Bongo falvour kuweza kuingia na kupata nafasi nzuri West africa... kama nilivyoahidi na kuzungumza mwanzo kuwa mwaka huu Moja ya Mission zangu ni kuhakikisha pia Muziki wetu unapata nafasi nzuri South Africa na America... tafadhali usiache kunisupport ili kwa pamoja tuufikishe mziki wetu Kileleni...) #MakeMeSing @akaworldwide X @DiamondPlatnumz Drops on Friday!

SASA RASMI;DIAMOND AFANYA KUFURU,KUTOA ELFU 50 KWA KILA MTU KISA JAMBO HILI TU,SOMA HAPA LIVEE..!!


Diamond ameandika haya kupitia ukurasa wake wa instagram

Kwa sasa nipo South Africa kikazi lakini wiki ijayo nikirudi tu Tanzania nataka nitoe zawadi kwa watu 30.... ambao watakuwa wako na line ya Vodacom ntawaekea Vocha ya Elf Hamsini 50,000/= kwa kila Mmoja na Internet ya Mwezi Mzima Bure!!!!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top