Umewahi kujikuliza kwanini vyombo vingi vya mawasiliano vinapiga miziki ya kukufanya usahau ulipotoka na unapokwenda.Tuangalia wasanii wengi wanaotoka nje kuja kufanya matamasha hapa nyumbani.Hawa wasanii nyimbo zao si za HASIA.Unaweza kulinganisha wanamuziki wa HISIA na hawa wengine?Mwanamuziki wa HISIA yuko makini sana,kuanzia kwenye mavazi na tungo zake.Lini tutasikia Mwalimu wa Afrika anatua Bongo?au tutazidi kuwakaribisha kina KC na 50cent au JayZ.Tukirudi nyumbani na kuwasiliza wasanii wetu,tungo zao zimejaa mapenzi,yani wanamuziki wanaabudu mapenzi kila kukicha utasikia sijui sinderela nakupenda,nakupenda nita n.k.Mwanamuziki anapaswa kuwa makini sana katika tungo zake,wewe mwanamuziki chini ya umri wa miaka 18 unaimba mapenzi inakuja kweli?Hivi katika tungo tunaangalia sauti au UJUMBE?Tusipokuwa makini tungo zetu zitaishia kuwa kama moto wa petroli.Upande wa blogu je?Kweli kabisa,inauma,inasikitisha kuona baadhi ya blogu zikiweka picha za maisha ya furaha,picha za vilevi huku mabinti wakiwa vifua wazi na miguu nje,inasikitisha kujitangaza wewe maisha yako au yenu ni mazuri katika chomba cha habari kama blogu.
Imeandikwa na Rasta Hapa.
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana