CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii
Idara ya Lugha na Fasihi- Kitengo cha Kiswahili
TAMASHA LA SAUTI YA KISWAHILI (TASAKI)
Lugha ya Kiswahili sasa imevuka mipaka ya kitaifa. Ni lugha ambayo imeshuhudia mageuzi mengi na imepiga hatua kubwa sana. Tunashudia watu wengi ulimwenguni wakijifunza Kiswahili na hata Vyuo Vikuu vikifundisha Kiswahili. Ni wakati ambao watanzania tunahitaji kukipa kipaumbele na kujivunia lugha yetu na utamaduni wake, kuipa nafasi na dhima maalumu katika nyanja zote za elimu, siasa, uchumi na utamaduni. Lugha ndiyo rasirimali pekee ambayo mtu anapaswa kuitumia ili kufikia maendeleo ya kweli. Ili uweze kumtawala mtu au taifa basi mnyang’anye lugha na utamaduni wake. Hivyo basi, utandawazi umekuja na upepo mkali sana mbao tusipochukua juhudi za makusudi tutakiona Kiswahili kikitupwa baharini na upepo huo. Ili kukumbatia lugha na utamaduni wetu yatupasa kujenga ukuta imara ambao hautatikisika kwa upepo wa utandawazi. Ukuta huo basi ndiyo TASAKI ya OUT. Kupitia TASAKI, sauti ya Kiswahili itasikika ndani ya nchi, Afrika Mashariki, Afrika na ulimwengu wote.
Katika misingi hii, TASAKI imeandaliwa katika muktadha unaowapa washiriki fursa ya kumulika na kutafakari mabadiliko na maendeleo ya Kiswahili katika dunia ya utandawazi ili kuleta uhuru na maendeleo ya kweli. Aidha TASAKI imekusudia kuwaandaa vijana na wananchi wote kuutambua ulimwengu wa Kiswahili na utamaduni wake. Kwa kufanya hivi TASAKI inaotesha mbegu ambazo zitazaa matunda siku moja kwa kuisimamisha nguzo ya Kiswahili ambayo ndiyo taa ya watanzania.
Hivyo basi, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinaandaa Wiki la Tamasha la Sauti ya Kiswahili litakalofanyika Novemba 2009. Hii itakuwa ni wiki ya kitaaaluma na burudani ambayo ina lengo la kutangaza, kueneza, kuendeleza na kuinua lugha ya Kiswahili na utamaduni wake katika dunia ya utandawazi.
Tamasha hili litahusisha wanazuoni, wanachama wa Kiswahili wa Afrika Mashariki na kati, Taasisi za Kiswahili, wanafunzi wa vyuo vikuu, Sekondari, wasanii na vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni, wadau na wakereketwa wote wa lugha na utamaduni wa Kiswahili ndani na nje ya nchi.
Katika wiki ya sauti ya Kiswahili kutafanyika makongamano, mashindano ya uandishi wa kazi za kubuni kwa shule za Sekondari, Vyuo Vikuu na watunzi wasio wanafunzi. Vile vile kutakuwepo na maonesho ya Sanaa na utamaduni; mavazi ya Kiswahili, vyakula vya Kiswahili, Majigambo, Ngoma, Taarab, Maigizo, Utambaji wa hadithi, muziki wa kizazi kipya na ghani za mashairi mbalimbali.
Tamasha hili litafanyika kila mwaka katika kituo chochote cha Chuo Kikuu Huria ingawa mwaka huu 2009 Tamasha hili litafanyika katika jiji la Dar es salaam.
Kauli Mbiu ya Sauti ya Kiswahili ni kueneza lugha ya Kiswahili na utamaduni wake kwa kuipa nafasi na dhima mahususi kitaifa na kimataifa.
Mada ya Sauti ya Kiswahili 2009 ni Nafasi ya Kiswahili katika Ulimwengu wa Utandawazi.
MASHINDANO!
Mashindano ya uandishi wa kazi za kubuni yatahusisha makundi matatu
· Wanafunzi wa Sekondari
· Wanafunzi wa vyuo vikuu
· Watunzi wasio wanafunzi
MADA KWA AJILI YA MASHINDANO YA UANDISHI WA KAZI ZA KUBUNI SHULE ZA SEKONDARI
Mada zifuatazo zitazingatiwa katika utunzi wa Mashairi, Riwaya, Tamthiliya, Tenzi na Ngonjera.
1.Lugha na elimu
2.Watoto wa mitaani
3.Ukimwi
4.Mauaji ya Albino
5.Lugha na mazingira MADA KWA AJILI YA MASHINDANO YA UANDISHI WA KAZI ZA KUBUNI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU
Mada zifuatazo zitazingatiwa katika utunzi wa Mashairi, Riwaya, Tamthiliya, Tenzi na Ngonjera.
1. Unyanyasaji wa kijinsia
2. Ukimwi
3. Watoto wa mitaani
4. Imani za kishirikina
5. Lugha ya Kiswahili na utamaduni wake
6. Lugha na ajira
7. lugha na demokrasia
8. Mauaji ya Albino
9. Lugha na mazingira
MADA KWA AJILI YA MASHINDANO YA UANDISHI WA KAZI ZA KUBUNI KWA WATUNZI WASIO WANAFUNZI
Mada zifuatazo zitazingatiwa katika utunzi wa Mashairi, Riwaya, Tamthiliya, Tenzi na Ngonjera.
1. Unyanyasaji wa kijinsia
2. Ukimwi
3. Watoto wa mitaani
4. Imani za kishirikina
5. Lugha ya Kiswahili na utamaduni wake
6. Lugha na ajira
7. lugha na demokrasia
8. Mauaji ya Albino
9.Lugha na mazingira
KONGAMANO!
Hapa kutakuwa na mada za kitaaluma ambazo zitajikita katika Isimu na Fasihi ya lugha Kiswahili. Dhamira mbalimbali zitajadiliwa katika kongamano. Dhamira hizo zitajumuisha mada zifuatazo
MADA ZA ISIMU
1.Kiswahili na demokrasia
2.Kiswahili na sheria
3.Kiswahili na utandawazi
4.Kiswahili na elimu
5.Kiswahili na utamaduni
6.Kiswahili na siasa
7.Ushiriki wa umma katika michakato ya kidemokrasia
8.Lugha na shirikisho la Afrika Mashariki
9.Tafsiri na ukuzaji wa lugha ya Kiswahili
10.Lugha ya Kiswahili na mahitaji maalum
11.Lugha katika sayansi na teknolojia
12.Leksikografia
13.Muingiliano wa lugha ya Kiswahili na lugha za kiafrika
MADA ZA FASIHI
14.Fasihi na masuala ibuka
15.Mikondo na mielekeo mipya katika fasihi ya Kiswahili
16.Fasihi na maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni
17.Lugha ya vijana
18.Fasihi na mazingira
19.Maendeleo ya Ushairi
20.Kiswahili na jinsia
21.Kiswahili na sanaa za maonenyesho, filamu na muziki
22.Lugha na ujasiriamali
23.Lugha na ukombozi
Washiriki wa kongamano watume ikisiri za makala zao kabla ya tarehe 20/08/2009
Washiriki wa uandishi wa kazi za kubuni watume kazi zao kabla ya tarehe 20/9/2009
Karibuni sana tushirikiane katika kuienzi, kuieneza na kuitangaza lugha ya Kiswahili na utamaduni wa kitaifa
Aidha, Ikisiri zote na kazi za kubuni zitumwe kwa barua pepe na anuani zifuatazo;
1. Mkuu wa Kitivo cha Sayansi na Sanaa za Jamii
Chuo kikuu Huria cha Tanzania
S.L.P 23409
Dar es Salaam
Tanzania
Barua pepe: dfass@out.ac.tz
Emmanuel.mbogo@out.ac.tz
Simu ya mkononi: +255753420118
2. Mwenyekiti wa TASAKI
Chuo kikuu Huria cha Tanzania
Kitivo cha Sayansi na Sanaa za Jamii
Idara ya Lugha na Fasihi
S.L.P 23409
Dar es Salaam
Tanzania
Barua pepe: hadija.jilala@out.ac.tz
dijaah@yahoo.com
addhass@gmail.com
Simu ya Mkononi: +255712569555
Loading...
TAMASHA LA SAUTI YA KISWAHILI (TASAKI)
Post a Comment
CodeNirvana