WABUNGE wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, wamesema Tanzania haijui inafanya nini katika jumuiya hiyo na kwamba hiyo inatokana na kutokuwa na mipango madhubuti ya kutumia fursa mbalimbali zilizopo.
Wabunge hao walisema hayo jana, walipokuwa wakijibu maswali ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayooingwozwa na Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa.
Mmoja wa wabunge hao, Janet Mmari, aliiambia Kamati ya Lowassa kuwa Tanzania haijui inafanya nini katika jumuiya hiyo na kwamba hiyo inatokana na kushindwa kujipanga kama inavyofanywa na nchi nyingine.
Alisema nyingine za jumuiya hiyo zimejipanga vizuri na zimekuwa zikiwasaidia wabunge wake."Serikali ya Kenya imejipanga kuwaeleza wananchi wao na kutumia vizuri fursa za jumuiya. Sisi bado tupo nyuma na hata bajeti yetu ni 'kiduchu',"alisema Mmari.
Aliiomba kamati hiyo iwasaidie ili waweze kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa kuwa nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo, zimejipanga katika kuwasaidia wafanyabiashara wao, kutumia vizuri soko la pamoja.
Sebtuu Nassoro, alisema tatizo kubwa ni kwamba Tanzania kushindwa kujipanga ndani ya jumuiya hiyo na hivyo kusababisha isijuie inachokifanya."Hatujajipanga ndiyo tatizo letu, ndani ya jumuiya,"alisema Nassoro.Dk Amani Kabourou, alisema kuwa Tanzania hakuna elimu yoyote inayotolewa kuhusu nchi nyingine zinavyofanya kufanikisha mambo yao, ndani ya jumiya.
"Huwa hatuna mkutano na waziri mkuu wala rais, kama ilivyo kwa wenzetu wa Kenya ambao huwa wanakaa nao na kupanga mikakati kwa kuwa wanajua wanachokitaka,"alisema Dk Kabourou.Kwa upande wape, Dk Didas Masaburi, alisema wabunge wa Tanzania hawajui wanaripoti wapi baada ya kutoka katika Bunge la Jumuiya.
"Ni wakati muafaka sasa kujua sisi tunaripoti wapi, hatuna usafiri wala mwandishi hata hii taarifa ni mwenyekiti kaandaa mwenyewe,"alisema Dk Masaburi.
Alisema hajawahi kuona Bunge linaripoti kwa wizara kama inavyofanyika hapa nchini kwa wao kuripoti katika Wizara ya Afrika Mashariki.Dk Fortunatus Masha, alisema kuwa Tanzania iko nyuma sana kwa kuwa wananchi hawana elimu ya kutosha kujua nini wanapaswa kukifanya.
"Elimu kwa wananchi tuko nyuma, wananchi lazima waelimishwe kuhusu masoko ya nchi hizi,"alisema Dk Masha.
Wakati akitoa taarifa yake kwa kamati hiyo, Mwenyekiti wa wabunge wa jumuiya hiyo, Kate Kamba, alisema umuhimu wa Tanzania katika jumuiya hiyo ni kuwa na bandari kubwa.
(Habari na Boniface Meena,Mwananchi)
Loading...
1 maoni:
Wakubwa wanasema hivyo ni kazi kweli mkuu !!
Reply