Katika pitapita yangu kusoma habari mbalimbali zilizojiri na zinazojiri nikakutana na Blogu ya G Sengo kuhusu kisa hiki bungeni nauita utamu wa Bunge hili kumbe twakosa mengi Hebu jisomee....
Niliidaka juu kwa juu tu! leo katika mjadala wa kupitisha Hoja moja wapo kuelekea mchakato wa kupata wawakilishi wa Bunge la Afrika kupitia televisheni LIVE na nikakuta Mbunge wa Nyamagana Mh. Ezekiel Wenje ndiye alikuwa amesimama akitoa pendekezo nao wabunge wenzake wakimzodoa.
Mara sauti zikasikika na nilizozinasa ni hizi;
*****-"akanywe kikombe cha babu huyo...!"
*****-"futa kauli!"
*****-"we vipi waambiwa huna maskio!"
*****-"jamani hatuko klabu tuko bu-nge-ni!"
*****-"out!out katuburuza huyo!!"
SPIKA: "jamani naomba utulivu!!"
*****-"hatoki mtu nje!!"
*****-"tutatoka wote....!!!"
*****- "tufunge mlango tupigane!!...!!"
(***)-"naona mnafanya mnada badala ya kuendelea na bunge"
*****-"msitumie wingi wenu kutuburuza!!"
SPIKA: "watu mmechaguliwa na kura za wananchi kwanini mwafanya mambo ya kitoto hivi hamjui kuwa tunaonwa na wananchi?...!
Ndipo atilisti utulivu ukapatikana uchaguzi wa Pan Africa Parliament ukaendelea....
(Habari kwa Hisani ya G Sengo)
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana