Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewataka wanafunzi waliotuma maombi ya kujiunga na vyuo vikuu kupitia tume hiyo kuwa na uvumilivu kwani majibu yatatoka hivi karibuni.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Afisa Uhusiano wa TCU, Edward Mkaku, alipozunguumza na NIPASHE ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi kuhusiana na malalamiko ya wanafunzi walioomba nafasi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwamba tume imechelewa kutangaza majina.
Mkaku alisema kwa kawaida matokeo ya waliochanguliwa kujiunga na vyuo vikuu nchini hutolewa mwishoni mwa Julai. Hata hivyo, alisema mwaka huu majina yamechelewa kutangazwa kwa kuwa seneti za vyuo zimechelewa kufanya vikao kwa ajili ya kupitia na kuhakiki majina na sifa za walioomba.
Alisema kazi ya TCU ni kuratibu na inapomaliza humuita Afisa Msajili wa kila chuo kwenda kuangalia kama wanafunzi waliochanguliwa wana vigezo vya kujiunga na chuo husika kwani kila chuo kina kuwa na vigezo vyake.
Aliongeza kuwa baada ya kila Afisa Msajili kuhakiki vigezo vya waliochanguliwa, huenda kukaa na Baraza la Seneti la kila chuo kuhakiki tena vigezo hivyo na baada ya hapo majibu yanarudishwa TCU.
Mkaku alisema TCU ilikutana jana na kwamba wakati wowote itatoa majibu ya waliochanguliwa kujiunga na vyuo vikuu.
Aliongeza kuwa TCU ina mawasiliano ya vyuo hivyo ambavyo ni taasisi huru.
CHANZO: NIPASHE
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana