Salaam nyingi kweni nyi wote wapenzi wa muziki hapa Bongo,leo kamanda wenu Mac Temba aka mwanaharakati wa Anti virus nataka kuwapa tafsiri na kuweka mambo sawa yote kuhusiana na mambo kibao yanayopindishwa na kuficha ukweli wa Vuguvugu la kudai haki sawa na uwanja huru wa kufanya sanaa hapa Bongo,kwa jina la mtaani limepewa jina la “Anti virus”
Anti virus ni mkusanyiko wa watu mbalimbali wenye taaluma mbalimbali na uwezo mbalimbali ambao tunaamini kuwa sanaa hii ya muziki inaweza kuwasaidia vijana wengi hapa bongo na pia kuisaidia nchi yetu kupata kodi ambayo itasaidia kuleta maendeleo na kuisogeza nchi yetu mbele kama wenzetu Afrika kusini,Nigeria.Kamwe huu si mgomvi na mtu mmoja wala chombo kimoja cha habari.
Kinachodaiwa hapa ni haki na usawa katika sanaa na malipo sahihi kama wanavyolipwa wakenya na wanaigeria wakija hapa kufanya maonyesho mafupi ya muda wa saaa moja na kuchota mamilioni mengi toka kwa makampuni ambayo yanapata faida toka kwa watanzania hawa ambao wasanii wao wa ndani wanaishi maisha mabovu sana na wala hawakumbukwi na makampuni haya ya bidhaa ambayo hupata mamilioni ya faida toka wa watanzania hawa.
Sanaa na soka ni fursa pekee ya kumfanya mtoto toka katika familia masikini kuweza kuwa milionea ama kufanikiwa kujinyanyua toka katika maisha mabovu mpaka maisha bora,ni kama mpira ulivyo katika nchi ya Brazil,soma historia za wanasoka kama wakina Ronaldo de Lima na wekina Pelle soka ndilo lililowafanya waweze kujiinua na kuweza kuzisaidia familia zao kupata mafanikio na kuishi maisha bora nay a kifahari.
Hakika naomba niweke sawa hapa Anti virus movement ya kudai haki si ugomvi kati ya Sugu na Ruge bali ni vuguvugu la wasanii wa zamani wanaamini kuwa game ya muziki haiendi sawa na kutaka mambo yawe wazi na BASATA na COSOTA kuundwa upya ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupunguza haya malalamiko na pia watu hao wanaoitwa mapebari katika muziki(hao Virusi katika muziki wanaotafuna mamilioni ya wasanii wetu wachanga wakome),hii ndio sababu ya anti virus na hakika kadiri muda unavyozidi kwenda nashukuru watanzania wanazidi kutuelewa.
Sugu ndiye msanii pekee anayeweza kusimama mbele na kujiita Legendary katika muziki huu na si mwingine yeyote maana wengi wao ni kama “fisi maji” mnaotaka mabadiliko lakini hamtaki kuongea eti “mtanyimwa airtime redioni” acheni ujinga na kujifanya wanaharakati wakati mnaendelea kunyonywa na mnaishi maisha mabovu wakati sanaa yenu ni kubwa sana na ndiyo kazi pekee inayowafanya muishi mjini,maana wengi wenu mliacha shule kukimbilia katika sanaa cha kushangaza mnaogopa kusimama na kutetea haki zenu za msingi.
Mapambano dhidi ya vuguvugu la kupinga unyonyaji huu hayajaanza jana wala juzi,Solo Thang mwana hiphop anayeishi na kufanya kazi Ireland aliwahi kuingia katika beef na redio moja hapa kwa kudai haki na kuwachana kuwa wanaiba haki za wasanii,wakampiga vita na kumtengenezea kila hila ili kumpoteza,hata wasanii ukiongea nao wanajua haya ila eti wanamuogopa huyo virus eti atawapoteza na kuwanyima airtime ila wako tayari kuendelea kusafriki mikoa yote kwa show ya laki 4 wakati wanaingiza mamilioni ya shilingi.
Inashangaza eti msanii kama Lina eti anaambiwa ana mafanikio kwa kuweza kununua gari aina ya “Vitz” baada ya kuuza albamu na kufanya show kibao,je haya ni mafinikio kweli kwa mauzo ya albamu Bongo?haya ndio mambo tunayopigia makelele maana zamani adui wa wasanii alikuwa mdosi lakini siku hizi mpaka huyo Virus sasa ndiye anayeamua kusambaza albamu za wasanii wetu na nani apewe shilingi ngapi kwa albamu yake.
Ni wasanii wangapi wa hapa kwetu wenye kuishi maisha ya kueleweka na kumiliki vitega uchumi na kuweza kuendesha maisha yao???hakika hawazidi kumi kwasababu wengi wanapambwa redioni lakini ki uhalisia hawana cha maana,hebu ona wsanii kama Mr Nice,Bushoke,Gangwe Mobb,Feroos,East Coast Team walivyotumiwa na alivyotupwa na hao wadau,Sio kwamba wametumia pesa vibaya bali asilimia kubwa ya pesa hizo huliwa na hao wadau na kuahidiwa eti promotion ya albamu ijayo.
Hili si sawa ndio maana katika hili tunataka wanaojibu hoja za Anti virus wajibu hoja na sio propaganda za kitoto maana watu wameamka na wanataka majibu na uwanja huru katika sanaa,kila mwenye fursa na uwezo katika sanaa afanye bila kubughuziwa,sanaa iwe huru na vyombo vinavyosimamia sanaa viweze kufanya kazi bila mikono ya hawa virus aka mabepari wa sanaa wanaopigwa vita.Huu sio ugomvi wa watu wawili hapana,haya ni mapambano ya kudai haki na usawa katika sanaa yetu maana sanaa si ya watu wachache.
Kama mambo haya ya sanaa yetu yangeweza kuwa wazi na fair tungeweza kuwa na wasanii wenye mafanikio kama lady Jaydee wengi sana na hakika wangeweza kuwavutia mabinti wengi kuingia katika sanaa hii lakini ukimtoa lady jaydee taja mwanamuziki mwingine mwenye mafanikio kama yeye,Kuna siku moja niliona mahojiano na msanii mmoja mkubwa wa hip hop bongo anayejiita legendary akisema mafanikio yake katika gemu toka aanze miaka zaidi ya kumi nyuma ni nyumba na gari Spacio!!! Daah inasikitisha sana unapoona msanii kama Nonini wa juzi juzi sasa hivi ana mafikio makubwa na hafanyi show chini ya dola 2500 na ukiwataka P unit ni dola 3000 lakini katika show hiyohiyo msanii wa bongo analipwa laki 4 na wengine mpaka bure kwa ahadi ya kupewa airtime redioni kwao,huu ndio wizi tunaousema uishe maana ni lini msanii wetu atakuwa na mafanikio kama malipo ndio haya.
Hofu kubwa ya kundi hilo la mafisadi wa sanaa hapa Bongo ni kuwa haya mambo yakiwa wazi watakosa pa kuiba na kufisadi ndio maana wanapandikiza mamluki na kujibu majibu ya ki propaganda na kukimbia hoja za msingi,jambo moja ambalo wanapaswa kulijua ni kuwa hakuna jambo ambalo halina ncha.
katika hili muda umefika,jana kwenye facebook mambo mengi yamejiri na comments kibao mmoja wa wadau wa muziki Pkay alindika “the fall of Roma empire…wake up kids…maji yakizuiwa njia hutafuta mkondo mwingine,someni alama za nyakati”
Dada Maria Sarungi- Tsehai yeye aliubatiza huu mwamko kama Sugu phenomenon katika ukurasa wake wa facebook jana na kusema “Angry young men ambao wamechoka na wameamua kujiexpress kupitia muziki,ni hatua nzuri ila isiishie hapo…”
Carren Flora Mgonja kwenye wall yake ameeandika”Asanteni vinega kwa kutupa show tukioikosa kwa long tyme,I salute my brothers,safi sana Adili na songi lako peke yangu,Soggy na kibanda cha simu”
Hili mimi nililijua litafika hapa maana hakika ni jambo ambalo tulikiwa tunalizungumzia mara kwa mara katika mijadala na wadau wa muziki huu kuwa kuna watu wachache wanaohodhi mamlaka na kufanya mambo katika sanaa yasisogee mbele kwa manufaa yao binafsi,napinga sana suala hili “eti muziki wetu haulipi”nani kasema muziki haulipi?mbona hao wadau ni muziki huu huu umewafanya mpaka wameweza kufungua TV,muziki huu huu ndio unaowafanya wao kununua magari ya kifahari.
Nguvu ya mabadiliko ya watu haipingwi kwa vijembe redioni wala maneno ya shombo,bali kwa Hoja zenye msingi na zenye majibu na si kwa hoja nyepesi jamani,wasanii wengi wamejazwa fikra kuwa huu ni ugomvi binafsi kati ya watu wawili,hakika sio kweli,suala la Malaria No more limepita sasa tunasonga mbele na kutaka kila msanii kweli apate kipande chake halali na kuacha kutengenezewa wasanii na kikundi kimoja cha watu kwa maslahi yao.Miaka miwili iliyopita walianzisha mizengwe eti Hip Hop hailipi na kuwavuruga sana wasanii na wale wachache wasioweza kupambana wakaamua kuanza kubana pua ili wapewe airtime.
Kwa muda mrefu nimekuwa mdau na naufahamu muziki huu kwa upeo mkubwa sana na ndio maana nayaongea haya bila woga,ifike muda kila mtu akafanya jambo analolijua na sio kubahatisha,kuna jamaa mmoja eti ni “music director “wa redio moja hivi ya fm hapa mjini eti yeye kazi yake ni kusikiliza nyimbo na kutoa kasoro na marekebisho cha kushangaza huyo anayeitwa music director hana hata diploma ya muziki huo,unawezaje kukosoa kitu amabcho hukijui na kutenda haki???haya ndio mambo ya kimagumashi yanayoharibu muziki wetu,get a life boy na kama unataka kufanya mambo nenda shule japo diploma itakupa msingi wa kufanya hayo.
Miaka michache iliyopita alivuma msanii Mb Doggy na kutajwa kuwa ameuza kopi zaidi ya laki moja katika siku mbili za mauzo ya albamu yake ya “Lafifa”daah akapewa coverage kubwa na mengi yakasemwa ooh kavunja rekodi mpaka kawafunika jamaa wa bendi lakini hebu mtafute Mb Doggy leo kaa nae umuulize uhalisia wa yaliyotokea,utasikitika na kuduwaa,leo hii Mb Doggy anapambana kurudi upya kwenye game japo apate hela ya kuishi,hii ni hatari sana.
Wasanii wa bongo amkeni acheni kufanywa misukule na kutumiwa kama daraja la kupata mafanikio ya watu wachache na aminini kuwa hata nyie mnauwezo wa kufanya makubwa na kumiliki magari ya kifahari kama chameleon,Nonini,Bebe Cool ama Nameless na kuacha kuishi maisha ya kuunga unga wakati you got all the means to be on Top,Bila kuamka na kupigania hili hakika mtazeeka na kukosa la kuwaelezea watoto na wajukuu,Hata marehemu mzee Kipara wa kaole alikuwa kijana kama nyie hebu ona maisha ambayo alikuwa anaishi mpaka mauti ikamfikia.inasikitisha na bila kutumia ujana wenu sahihi hakika mtakuwa mizigo huko uzeeni.
Waraka wa pili utakujia tena jumatatu ijayo>>>>hii ni kwa ajili ya wapenda muziki wote na kupata ufahamu ya kinachoendelea kwenye Anti Virus Movement ya kuokoa muziki huu wa Bongo usiendelee kupotea na kufaidisha kundi dogo la mabepari aka Virusi.
ALUTA CONTINUA….
Anti Virus Activist -MAC
KWA HISANI YA karibundani.blogspot.com
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana