Loading...
Adha ya usafiri Yale yaleee..!!
Unapoamka asubuhi kuelekea kituo cha Daladala ili uweze fika mahala pa kazi huwezi jua mbele yako itakuwaje hapa naongolea usafiri wa kukufikisha kazini mwako au sehemu yako ya kutafutia mkate wa kila siku. Mara nyingi KAZI huwa namna ya kupata usafiri ili uweze fika salama huko uendako.Wengine huamua kupitia njia za panya ili apate kiti cha kukali kama mwenzetu hapo juu(taswira yajieleza) aliamua isiwe shida yanini yote hayo kupigana vikumbo mlango ilhali umbo langu laniruhusu pita hapa ? huyoooo mwanaume akajipinda dirishani kwani mlangoni wanasema unaweza pishana na vyako maana yake wewe unaingia ulivyonavyo mfukoni(simu na pochi au vijisenti vyako) vinachomolewa bila kujua na wewe kubaki huna kitu mfukoni.Basi hili utambue mapema unaweza japo omba konda akusafirishe hadi ushukapo au abiria wenzako kukusaidia hiyo nauli la sivyo unaweza jikuta Kondakta nae wakati anadai chake(nauli) akakuanzishia zogo jingine ilhali weye hukujua kama umeshapishana na vyako mlangoni ...!!
Niwatakie Ijumaa njema.
Endelea kutembelea Kijiweni Rundugai
Post a Comment
CodeNirvana