Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Fuso lagongana na Gari ndogo Iringa asubuhi hii barabara ya Iringa-Mbeya na kusababisha vifo.


Askari wa usalama Barabarani wakiondoa mwili wa mmoja wa waliofariki katika ajali iliyotokea asubuhi ya leo kati ya Gari dogo''Tax'' na gari kubwa aina ya Fusso ambapo watu watatu wamefariki dunia katika ajali hiyo.

Fuso lililogongana na Taxi katika barabara ya Iringa-Mbeya maeneo ya Ruaha Esso.

Watu wakiangalia gari ndogo iliyogongana na Fuso huko Iringa,Ruaha Esso barabara ya kwenda Mbeya likiwa pembeni mwa barabara hiyo.

Fuso hilo likiwa limechomoka tairi la mbele baada ya kugongana na gari ndogo

Hiyo ni Taswira ya Gari ndogo inayofanya biashara ya 'TAXI' likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Fuso.Taxi hiyo namba za usajili T620 ANE ilikuwa ikitokea Ndiuka ikiwapeleka wafanyakazi wa barabara katika eneo la Tanangozi ambapo ujenzi wa barabara ya Iringa-Mbeya unaendelea.

Hata hivyo kabla ya kufika katika eneo hilo la kituo0 cha Mafuta cha Eso dereva wa Taxi hiyo ambaye alikuwa akitaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele yake alishindwa kulipita gari hilo baada ya kukutana uso kwa uso la Fuso yenye namba za usajili T897 AQS ambalo lilikuwa limeshehena magunia ya mpunga .

Hivyo kutokana na mwendo kasi ambao Fuso hilo lilikuwa likienda nao na mwendo kasi wa Taxi hiyo uwezekano wa kukwepana ulishindikana na hivyo kupelekea fuso hilo kuigonga Taxi hilo na kuipitia kwa juu na kupelekea vifo vya abiria wawili na dereva wa Taxi hiyo papo hapo.....habari zaidi Mtembelee Mzee wa Matukio Daima toka Iringa.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top