Loading...
Joshua Nassari kutoa Sadaka ya shukrani Kijijini Kilinga
Kama mnavyokumbuka wakati wa kampeni slogan yangu ilikuwa "tulianza na Mungu, tutamaliza na Mungu". Ninaamini ya Kuwa Ubunge nilipewa na Mungu kupitia watu wa Arumeru mashariki. Nimekuwa jimboni tangu usiku wa siku lilipohairishwa bunge kwa sababu ya mambo Mengi Hususani sintofahamu ya Swala sima la Ardhi na tayari nimeshafanya mikutano Kwenye vijiji kadhaa.
Kwa sababu tulianza na Mungu na bado tupo na Mungu, jumapili ya tarehe 20 mwezi Huu nitatoa sadaka ya shukrani Kijijini kwetu Kilinga Meru. Ninawaomba wote ambao mtaweza kuhudhuria mshiriki pamoja tumshukuru Mungu.
Nassari J. MB
May 7, 2012.
Kutoka ukurasa wake wa Facebook.

2 maoni
Mkuu naona mambo yanakwenda vizuri,naona ujio wako mpya lakini mkuu huu ushauri ufwate,kwanza mkuu nakushauri blogu yako iwe ya kipekee,usiige kama blogu zingine zinavyofanya,tafuta habari,you need to be creative na kifaa unacho mkuu natuma habari humu ndani zitakuwa tofauti kwa sana.
ReplyAmani.
Tunashukuru sana mdau kwa ushauri tunaufuata vilivyo hilo ndilo TUNALIFANYA sasa ili mpate ladha tofauti
Reply