Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Lowassa awatuliza wana CCM wasihamie CHADEMA


Thursday, 10 May 2012 20:04
0digg
MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, amekuwa na mikutano ya ndani katika jimbo lake katika kile kinachoonekana kuwa ni jitihada za kutuliza wimbi la wana CCM kuhamia Chadema.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wanaCCM katika mikoa mbalimbali kuhamia Chadema. Mkoa wa Arusha ndiyo unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanachama wa CCM wanaojiunga na Chadema.
Jana Lowassa ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu, alifanya mkutano wa ndani katika eneo la Mto wa Mbu na baadaye kufuatiwa na mkutano wa hadhara.

Katika mkutano huo wa hadhara, mbunge huyo aliwaambia wananachi kuwa pamoja na kuwa suala la kujiunga na chama chochote cha siasa ni haki ya mtu, lakini haoni umuhimu wa wana CCM kwa sasa kuhama chama hicho kinachotawala.

Alisema CCM ni chama chenye kutetea maslahi ya wanyonge na kwamba kuna haja kwa wananchi kutathimini ili kuona kama kweli CCM imeshindwa kutimiza malengo yake.


Alisema CCM imekuwa ikitekeleza kwa vitendo mchango wa Baba wa Taifa Mwalimu Jiulius Nyerere ambao nni umoja na mshikamano, vinavyoifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.
Lowassa pia alisema CCM ni chama kinachotetea maslahi na rasilimali za nchi ili zisiporwe na wageni.

Amewakumbusha kuwa CCM ni chama kinachotoa nafasi kwa wanachama wake kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila ya mizengwe au ubaguzi wa rangi, ukabila au dini.

NA Mwananchi
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top