Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Manchester United walikuwa tayari kusherehekea kabla ya City Kusawazisha na Kufunga Goli la Ushindi.


Huku mchezo wa City na QPR ukiendelea na City wakiwa nyuma kwa 1-2 QPR maandalizi upande wa pili yalikuwa yanaendelea Pale United walipokuwa wanakipiga na Sunderland huku wakiwa wamesha watandika goli 1-0.

Wakiunganisha jukwaa dakika za mwisho wakitumaini Bingwa atapatikana hapo kwa Man United kutawazwa mabingwa ngoma iliyobadilika dakika za nyongeza na kuwa City ndio mabingwa wapya baada ya miaka 44 ya ukame wa kombe hilo.

Wangelala City au kutoa droo basi bango hilo lingekuwa ndilo lingetolewa wakati wa kusherehekea ubingwa huo lakini mwaka huu haikuwa hivyo.

Mashabiki wa Man United waliokuwapo Uwanjani hapo dhidi ya Sunderland wakishangilia wakati huo mahasimu wao City walikuwa wameshafungwa goli QPR 2-1 ya City.

Baada ya muda wakaduwaa baada ya kupata habarikuwa City wamechomoa na kupiga goli la Ushindi wakawa sasa sherehe yao imeingia mdudu kilichobaki kurudi nyumbani kwani Man City ndio Mabingwa wapya wa EPL.

Kocha na wachezaji wa Man United wakiwa hawaamini baada ya kupata habari kuwa Man City wamepata Goli la Ushindi hivyo kuwa Mabingwa wapya kwa msimu huu wa EPL furaha yao ambapo walikuwa tayari walishamaliza pambano lao na Sunderland na kuwafunga goli 1-0 huku wakisubiria dakika bili zilizobaki kwa mechi dhidi ya Man City na QPR iishe hapo City walikuwa wamesawazisha ambapo matokeo yangebaki hivyo United ingekuwa Bingwa lakin ikiwa ni dakika ya 3 sekunde 20 Man City wakaandika goli la tatuna la ushindi.Hivyo kufuta kabisa sherehe ambayo ilianza andaliwa hapo Uwanja wa Light.

Sir.Alex Ferguson kiutu uzima akaingia uwanjani kuwaongoza wachezaji wake na jopo lake la ufundi kuwashukuru mashabiki wa United kwa kuja kwao hapo uwanjani kushuhudia mtanange huo ulioishia kwa Sunderland 0-1 Man United.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top