Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Moto wa nyikani umewashwa


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezindua harakati za mabadiliko hivi karibuni jijini Dar es Salaam unaojulikana kama ‘Movement for change’ (M4C)’ wenye lengo la kuchukua nchini mwaka 2015.

Katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Jangwani, viongozi wa Chadema wamefafanua maana ya harakati hizo, wakisisitiza kuingia Ikulu 2015.

Akizungumzia kampeni hiyo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema kuwa kuna gharama kubwa kuiondoa CCM madarakani.

“Kila mwananchi anawajibu wa kubadilisha maisha yake. Kila mtu anapaswa kuwa wakala wa mabadiliko. Kuiondoa CCM kuna gharama kubwa, kule Arumeru walichanga thumni zao na kila walichokuwa nacho na hatimaye tulishinda, au siyo? Tusije tukapata viongozi kwa fedha chafu” amesema Mbowe.

Ili kuhakikisha kuwa chama hicho hakiingiliwi na mamluki, Mbowe pia amesisitiza kuwa watakuwa makini na wanachama wapya wanaohamia Chadema akisema kuwa watatakaswa kwanza kabla ya kupewa uanachama.

“Kuna watu wamekuwa wakisema kuwa eti tunachukua wasaliti wa chama. Ngoja niwaambie, tutakuwa makini na kila mtu anayehamia Chadema na tutafanya kama Mungu, kwanza tutawatakasa na kuwasamehe” amesisitiza Mbowe.

Ameongeza kuwa chama hicho kimejengwa kwa zaidi ya miaka 20 na kimeweza kujenga ngome katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Kuhusu vitisho vya jeshi la Polisi Mbowe huku akinukuu kauli ya Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliyoitoia miaka ya 1960, amelitaka Jeshi hilo kutowatisha wanachama wake kwakuwa kwa kuifanya hivyo wananchi nao watajibu mapigo.

“Chadema kitakuwa chama cha mwisho kuvuruga amani nchini. Nawaonya kama kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na kama Mwenyekiti wa Chadema na kama Mbunge. Nawaomba polisi, waache kuwasumbua wana Chadema” anasema Mbowe.

Kwa mujibu wa Mbowe, mikutano kama hiyo itaendelea katika mikoa ya kusini na hatimaye nchi nzima ili kukijenga chama.

Mchakato wa Katiba mpya
Katika mkutano huo, pia, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amewakumbusha Watanzania kuwa makini na mchakato wa Katiba ambapo ameibua hoja wanazopaswa kuzohoji wakati Tume ya Katiba itakapofika kutaka maoni yao.

Lissu amenza kwa kuikosoa Sheria ya kuunda Katiba akisema kuwa imezuia kuhoji masuala muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Amehoji masuala ya muungano ikiwa ni pamoja na nchi ngapi katika muungano.
“Waulizeni, tuna nchi ngapio katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Tuna wakuu wangapi katika nchi hii? Tuna maamiri jeshi wangapi? Tuna Jamhuri ya muungano wa Tanzania au ni kiini macho tu?” amsehoji Lissu na kuongeza,

“Nasema hivyo kwa sababu, wakati tunajuwa kuwa tuna Jamhuri ya Muungano, Katiba ya Zanzibar inasema Zanzibar nayo ni nchi. Wakati tuna Rais wa muungano, Zanzibar nayo ina rais. Wakati Rais wa muungano ni amiri jeshi wa majeshi ya ulizni na usalama, Rais wa Zanzibar naye ni mkuu wa idara maalum ambayo tunajua wana majeshi yao.”

Lissu amewataka wananchi kudai kura ya maoni kuhusu muungano na kudai Serikali ya Tanganyika.

Lissu pia amekosoa mchakato wa Katiba akigusia Bunge la Katiba na kusema kwa utaratibu uliopo litatawaliwa na wabunge wa CCM.

“Kwa utaratibu wa sasa Bunge la Katiba unaoruhusu wabunge wa vyama kuingia, litatawaliwa na wabunge wa CCM na CUF. Wabunge watakuwa zaidi ya 400, sisi Chadema tutakuwa 48, hatutafanya lolote. Matokeo yake mambo yatakuwa yaleyale.”anasema.
Ameshauri kuwa Bunge la Katiba lisihusishe wabunge wa vyama vya siasa, bali wananchi wote kwa jumla wahusishwe.

Kuhusu utaratibu wa kura za maoni, Lissu ametilia shaka utendaji wa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) akisema.
“Tatizo katika kura ya maoni ni Tume itakayosimamia, tume ya uchakachuaji ya CCM, mwishowe Katiba itapitishwa ki CCM, CCM tu. Tusiposimama na kupiga kelele mabadiliko ya Katiba, mambo yatakuwa yale yale.”

Amemtaka Rais Jakaya Kikwete kukumbuka makubaliano yao waliyokubaliana walipokutana Ikulu mwaka jana.

“Tulikubaliana kua mabadiliko ya Katiba hayataletwa na Tume hii ya uchaguzi. Jukumu la wabunge ni kukumbusha. Suala la muungano lipewe kipaumbele na namna nzuri ya kulinda muungano ni kudai Serikali ya Tanganyika.

Kuhusu madaraka ya Rais, Lissu amesema Katiba imempa madaraka makubwa kiasi kwamba anaweza hata kuuza nchi na asiulizwe.

“Hatutaki tuwe na rais wa aina hii, rais anayeteua wakuu wa majeshi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya. Tunataka tuwe na mfumo utakaomwajibisha rais.” anasema.

Ameshauri pia kuongezwa nguvu kwa mhimili wa Bunge akisema kuwa Rais amekuwa akiingilia nguvu zake.
“Mamlaka za utungaji sheria kama Bunge hazina madaraka, kwa sababu wabunge wengi hawakuchaguliwa na wananchi. Wengine wameteuliwa na rais, wengine viti maalum. Kuna zaidi ya wabunge 120 wasiochaguliwa na wananchi kati ya jumla ya wabunge 357. Ndiyo maana wamekuwa mafundi wa kupiga viti na meza.”anasema.

Ameshauri pia Bunge lipewe uwezo wa moja kwa moja wa kuiwajibisha Serikali.
“Mmeshuhudia hivi karibuni, mawaziri wametajwa kwa wizi. Kila mbunge amesimama na kuwawataja, lakini nani wa kuwawajibisha. Hadi Rais aje kuamua” anasema Lissu.

Lissu pia ameongeza kuwa kwa mfumo uliopo, wananchi hawana haki ya kumiliki rasilimali zao kama vile madini, ardhi na nyinginezo nyingi.

Gharama za maisha na madaraka ya Rais
Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama hicho Dk Wilbrod Slaa amewataka wabunge wa chama hicho kupeleka matatizo ya wananchi Bungeni hasa suala la kupanda kwa gharama za maisha.

“Maisha ya Watanzania si mazuri, gharama za vyakula zimepanda. Siku hizi hata maharage yamepanda, nyama, mchele, mkate na hata chai. Natumia nafasi hii kuwaeleza machache wabunge wangu ili wakayaseme bungeni, wabunge wetu hawana wa kuwafunga mdomo, maisha yamekuwa mazuri kwa mafisadi tu,” anasema Dk Slaa.

Akifafanua zaidi, Dk Slaa anasema mfumuko wa bei umepanda hadi asilimia 20 huku suala la ajira kwa vijana likiendelea kupigwa danadana na kuwategemea wawekezaji kutoa ajira.

“Serikali inaogelea kwenye anasa, Rais maeongeza baraza la mawaizir kutoka 50 hadi 55 na wotewanatumia kodi za Watanzania.” anasema Dk Slaa na kuongeza,

“Tulipokuwa tukizungumzia suala posho, hatukumaanisha posho za safari, hiyo hatujakataa. Ila posho za vikao. Kama wanalipwa posho za kukaa, basin a walimu walipwe posho za kusimama, polisi nao walipwe posho za kusimama” anasisitiza.

Huku akitoa mfano wa kupanda kwa nei ya mafuta ya taa, Dk Slaa anasema kuwa serikali inawakandamiza wananchi.

“Kuongeza kodi katika mafuta ya taa ili watu wasichakachue mafuta ya dizeli ni mwiba kwa Watanzania…, hii ni sawa na hoja ya mwendawazimu, wanatakiwa kudhibiti uchakachuaji sio kupandisha bei” anasema.

Dk Slaa pia aligusia mchakato wa Katiba mpya akiwataka wananchi kutoa maoni yao kuhusiana na mamlaka aliyonayo rais kwa kuwa ndio yanayosababisha ugumu wa maisha kwa Watanzania.

Anasema licha ya Watanzania wengi kutoijua Katiba, wao ndiyo wanaipa mamlaka serikali iliyoko madarakani kwa mujibu wa Katiba ibara ya 8.

“Tunataka kurudisha mamlaka ya kweli kwa wananchi. Kwa nini maisha ni magumu? Ni kwa sababu Katiba imempa mamlaka makubwa rais hasa kwenye suala la fedha. Inapofika wakati wa Katiba, ni rais na baraza lake la mawaziri ndiyo wanaokaa na kupanga. Mnapoumia rais hahusiki.”anasema.

Ameongeza kuwa madaraka ya rais ni makubwa kiasi ambacho hata wabunge hawana mamlaka ya kubadilisha bajeti.

“Rais wetu wanaweza kuteua idadi anayoitaka ya mawaziri. Sasa ameteua mawaziri 55 na hakuna wa kuhoji. Uingereza, Waziri mkuu amepangia kuteua mawaziri 20 tu, sana sana akiongeza ni mmoja.

“Huko Afrika kusini Serikali imepelekwa mahakamani kwa sababu watoto wamefeli mahakamani. Kwetu huduma kama hizi ni za kikatiba lakini haturuhusiwi kudai”

“Rais halazimiki kushauriwa jambo lolote katika utendaji wake. Hata rasilimali zetu akiamua anaweza kuzitumia atakavyo. Chadema tunaposema tubadilishe Katiba hatumaanishi kuvunja sheria, ila tuweke ubinadamu katika Katiba.”anasema Dk Slaa.

CHANZO - Tanzania Daima
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top