Loading...
Sihitaji ufahari na ubishoo jimboni Meru Mashariki- Nassari
NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-MERU
MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari amesema kuwa yeye hataki mambo ya kifahari katika jimbo lake bali anaitaji kuwepo na mikakati mbalimbali ambayo itaweza kuwasaidia wananchi wake katika harakati mbalimbali za maendeleo.
Kauli ya Bw Nassari aliitoa mapema wiki hii katika eneo la Sakila ndani ya kituo cha watoto yatima cha African Orphanage wakati wa hafla kwa watoto hao na mmiliki wake.
Bw Nassari alisema kuwa ni aibu kubwa sana endapo kama ataendekeza zaidi ufahari wakati wananchi wake wakiwa wanateseka na changamoto mbalimbali za kijamii huku muda nao ukiwa unadhidi kunyongonyea.
Alisema kuwa kwa muda wake mwingi sana atahakikisha kuwa anajikita na matatizo ya kijamii ambayo yamekuwa ni kilio kikubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Arumeru Mashariki ambapo changamoto hizo zinaweza kuepukika endapo kama watakuwa na umoja.
“Mimi sihitaji ubishooo au ufahari ndani ya jimbo hili kwa kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao wanaendekeza zaidi ubishoo na ufahari huku majimbo yao yakiwa na shida sasa sasa mimi natangaza hadharani hapa kwangu hamna kitu kama hicho”aliongeza Bw Nassari.
Pia alisema kuwa kwa upande wa Magari ambayo nayo hutumika mara nyingi na viongozi hasa pale wanapopata ubunge kwa upande wake yeye atatumia usafiri wa Kawaida sana ambapo baadhi ya fedha atazielekeza jimboni.
“jamani leo mnaona gari ambao mimi ninalo ni lakawaida sana si gari la kifahari na hata mara nyingine mimi kama mimi huwa natumia hata usafiri wa pikipiki(TOYO)kwa kuwa siendekezi ubishoo zaidi ila naelekeza nguvu zangu nyingi katika kusaidia jamii”aliongeza Bw Nassari.
Naye mkurugenzi wa kituo hicho cha watoto yatima bw Nickson alifafanua kuwa viongozi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajijenga zaidi katika mitizamo ambayo itaweza kuwasaidia wananchi na wala sio kulumbana.
Bw Issangya aliwataka viongozi kuhakikisha kuwa katika nyakati za sasa wanajikita zaidi kwa makundi maalumu kama vile yatima na wajane kwa kuwapa misaada ambayo inalenga kuwasogeza zaidi mbele na wala sio kuwatenga kama ilivyo kwa baadhi ya familia.
Post a Comment
CodeNirvana