Loading...
Tweets za Masanja Mkandamizaji akiwashukuru sana nyie wote....
Masanja Mkandamizaji @masanjawani
Jaaaaaaaaaaamboooooooooo! Mfanye Mungu namba moja na hutakuwa wa mwisho! Kumekucha mwanawani!
Jumatano mwanana kabisa kabisa mwanawani. Lazima ukiamka asubuhi uwashukuru saaaana watu wako kwa kila jambo! #NawashukuruSaaaana
#NawashukuruSaaaana Wale mlioweka Twiga kwenye makontena mkawamuvuzisha, naona Kaga anawakaba koo! Sijui kitu gani tena mmeuza hatujastukia!
#NawashukuruSaaaana Dada zangu na mashostito wote mnaolamba pete za uchumba kila musimu mwanawane! Mbarikiwe saaana
#NawashukuruSaaaana Mnaochomekea wenzenu barabarani bila hata kuomba mwanawani! Hivi unazani wenzako wameamka kuja pikiniki barabarani ama?!
#NawashukuruSaaaana Mnaozingua Zenji mwanawane wakati mnapataga supu ya samaki Mwanza na halua mnauza Kariakoo. Mbarikiwe saaaaana!
#NawashukuruSaaaana Mnaodisi wakaka wa Ki-TZ wakati ndo wamewamuvuzisha hadi hapo mlipo. Mito ya mibaraka iwatiririkie
#NawashukuruSaaaana Wote mlioleta keozi hadi nikashindwa kuchukua kiroba changu cha shokishoki na zaituni Mwanakwerekwe lasti wiki! Mnenepe!
#NawashukuruSaaaana Woooote mnaochukia watu bila misababu mwanawani. Kwa Malikia mnaitwa Hetazi. Baba awafanyie wepesi katika kazi yenu!
#NawashukuruSaaaana O-Bahama na wenzake wanaosapoti kale kamuchezo mwanawani! Mbarikiwe saaaana!
#NawashukuruSaaaana Wote mnaouliza "umekuja kufanyaje?" mkiwakuta watu supamaketi, "nimekuja kuvua samaki" mwanawan
#NawashukuruSaaaana Wooote mliomsaidia kijana wetu Sajuki mwanawane. Nawapenda saaaaaaaaana!
#NawashukuruSaaaana Woote mnaoua asili hadi ya majina mwanawani. We unaitwa Collins Mabula, mtoto unamuita Brown. Anakuwa Brown Collins!
#NawashukuruSaaaana Mnaofanya siasa kama biashara mwanawani. Mbarikiwe saaana na buku mbili mbili zenu mnazotupa. Nawapenda. Natania tu!
#NawashukuruSaaaana Wooote mnaopiga teni pasenti kimya kimya mwanawani. Najua mpaka ushtukiwe una tumbo na mishavu ya maana! Natania tu!
#NawashukuruSaaaana Woote mnaokaa kwa mashemeji bila kujishughulisha. Naona shemeji katoka kwenda kukutafutia asubuhi! Rilaksi tu hapo!
#NawashukuruSaaaana Wadosi mnaozingua wasanii. Mzidi kunenepa kwa kula mipilipili, pariki na kutema mate mwanawani.
#NawashukuruSaaaana Wote ambao hamjaoga asubuhi halafu kwapa unanyanyua juu kwa daladala! Levo yako ya konfidensi iko juu mwanawani!
#NawashukuruSaaaana Wote mnaotumia nafasi zenu na uwezo mliojaaliwa kupiga tafu wengine wasimame vizuri. Hatuna cha kuwalipa!
#NawashukuruSaaaana Na sina cha kuwalipa mnaoandika propozo feki mlambe mijehela. Ona mimacho ilivyokutoka!
#NawashukuruSaaaana Woooote mlio na mioyo ya kuvua soksi sebuleni kwa watu wakati mnajua miguu inatema smeli mwanawani! Ona ulivyoshtuka!
#NawashukuruSaaaana Wooote mliopigwa chini kwenye likabineti la mwanamkubwa kwa kukwapua halafu mkaenda kupiga pati! Tupeni chetu!
#NawashukuruSaaaana Woote mnaolipa wafanyakazi hewa. Yaani unamlipa mtu aliyeresti ini pisi? Iko siku atakutokea kwenye ei ti emu! Natania
#NawashukuruSaaaana Trafiki wote mnaoomba buku mwanawani. Hali imekuwa mbaya, yale mambo ya msimbazi acheni kabisa!
#NawashukuruSaaaana Woote mnaosema, "Jay - Z shwaini, Beyonsi mbaya tu." Piga kelele mwanawani, hasikiii na miziki hata hununui!
#NawashukuruSaaaana Woote mnaopiga fereee! Acheni walau kupulizia watu limoshi mwanawani!!
#NawashukuruSaaaana Wooote mnaowachomolea watu saidi mira pale Jangwani na Tazara, iko siku ntawachomoa makoromeo na mibange yenu!
#NawashukuruSaaaana Tigo. Siongezi neno!
#NawashukuruSaaaana Lile gazeti lilitumia picha ya mwaka jana ya Mtwara likasema ni ya lasti wiki ya Zanzibar. Pakinuka utauza gazeti??!!
#NawashukuruSaaaana Woote mlioko maabara mnakomaa na utafiti ili mwisho wake tuweze kupata chakula mtandaoni kama tunavyopata miziki na muvi
#NawashukuruSaaaana Wooote mnaotumia dini na ukabila kutaka kutenganisha watu! Pakinuka kikwelikweli hakutakuwa na ibada wala ngoma hapa!!
#NawashukuruSaaaana Mnaoanzisha vituo kulelea watoto yatima halafu mnalamba misaada! Ona tumbo lilivyokuvimba na bulakiberi yako!
#NawashukuruSaaaana Mawakili wooooote mnaojua kabisa mteja atashindwa kesi lakini hamsemi. Nawatakia biashara njema. Msijali, naelewa!
#NawashukuruSaaaana Marefa ambao timu zenu zinajulikana waziwazi. Tunakuwa hatupati taabu sana mwanawani!
#NawashukuruSaaaana Mlioaga tangu J3 kwamba mnakwenda safari za kikazi mkoani kumbe mko kwa nyumba ndogo mwanawani! Iko siku! Muone!
#NawashukuruSaaaana Kwa moyo wa uvumilivu na imani ya hali ya juu woote tunaotoa muvi 8 kwa mwaka na bado mambo hayasimama. Baba atatenda!
#NawashukuruSaaaana Wooote mnaonuna bila sababu
#NawashukuruSaaaana Mnaomiliki baa Soweto Moshi mlioamua kuwauzia watu Mtura kwa nyama ya mbwa mwanawani! Hivi mna nini vichwani?!
#NawashukuruSaaaana Singo mazaz mwanawane! Mnafanya meeengi makubwa! Mbarikiwe saaana.
#NawashukuruSaaaana Wauza chipsi mnaopasha moto mzigo uliobaki juzi na jana ili mtuuzie tena leo halafu nyie mnakula ule wa leo! Nashukuru!
Na Sisi KIjiweni Tunakushukuru sana Bwana Masanja Mkandamizaji kwa kutupa habari ya post kwa Blogi leo mwanawani.Mfuatilie twitter...Masanja Mkandamizaji @masanjawani
Post a Comment
CodeNirvana