Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Katika kupekua maktaba yetu ya Taswira tunakuletea hizi za wekundu wa Msimbazi wakiwa Kitaa cha Mbagala

Mwanadada hakusita kuficha hisia zake hapo akaona nae atoke na kuwapagawisha Watu waliokuwa wakishangilia msafara huo Hapo ni vingoma tu kwa ndni humo ya gari wana kidedea kama kawa.
Ishara ya kuchinjaa ilikuwa ndio kama nyumbani mtani kafungwa teena goli hizo zoote hivyo hapo wana sema tumekuchinjaaa...

Hawa nao huwa hawakosekaniii kila jambooo...Uzuri sherehe iliisha salama.



Nyomi hilo lilikuwa si la kawaida kila mmoja akitaka kwenda shuhudia hukoDar Live kutakuwaje.Hivyo gari hizo zilikuja na wapenzi wengi wa Simba ambao kila walipokuwa wakipita ilikuwa ni shangwe.



Humo ndani zilikuwa zikipigwa ngoma za wenyeji wa Pwani hivyo burudani ilikuwa mwanzo mwisho.Wanazi hao wawili wakiwa na furaha tele wao waliamua cheza kwa nje huku wakiwa ndani ya gari.
Hapo chachaaaa....Manyanga ilikuwa kama kawaida...mtani tena kabamizwa yakosekanaa ??? Chezea.


Taswira hii hapo walikuwa wakiwapongeza Watani wao haaswa aliekuwa Mwenyekiti Ndg.Nchunga kwa uamuzi wake wa kujiuzulu kwa kummwagia sifa kuwa kaona mbali kwani ameepuka lawama huku wakichagizwa na vingoma vya jadi vilivyokuwa ndani humo huku walioko mlangoni wakikata mauno kuonyesha furaha yao.
.....................................................................................................................................
Hizo ni Taswira Kijiwe ilizozipata wakati Simba walipoenda Dar Live tarehe 27/5 Jumapili iliyopita hapo ikiwa ni Mbagala kabla ya kuingia ndani ya ukumbi Tunatumaini umeburudika hiyo ni toka katika Maktaba Yetu.





author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top