Loading...
Machinga na mizigo yake kama msafiri
Ukimuangalia unaweza sema ni msafiri anasubiria gari ifike aende zake au asubiria wenyeji wake waje mchukua ndio kashuka hivyo toka safari.Wanasema ndivyo sivyo huyo ni mfanyibiashara ndogondogo akiwa na mizigo yake akisubiria muda uende ili nae afungue bidhaa zake si wajua vita yao na mgambo si ndogo.Hapo ni Buguruni Kituo cha Chama kwa wale waendao Mbagala.Gongo la Mboto,Chanika na kwingineko kwa wale watumiaji wa kituo hicho wapafahamu.Mida ya jioni utawakuta wengi wa aina hii wakiwa wapo kama hawapo kumbe wanaangalia hali ya hewa ikoje hapo ili waweze panga Bidhaa zao chini mida hiyo ya jioni ambapo wanadai ndio muda mzuri kwao kwa biashara.Kipindi hicho wanasema Serekali inakuwa imelala Hivi nikweli Serikali inalala ?Mie nawe hatujui.Lakini hapo wao ndio wasema wenyewe weshalala ni muda wetu sasa kutamba hata njia kwa sie wapita njia kuwa ya kutafuta Wenyewe wanatafuta minoti.
Post a Comment
CodeNirvana