Loading...
Mh.Joseph Selasini kupitia ukurasa wake wa Facebook atoa neno la shukrani
....Kwa niaba ya Familia yangu napenda kuwashukuru sana ndugu, jamaa na marafiki wote waliotufariji na kuwa pamoja nasi katika kipindi kigumu cha maombolezo ya misiba ya Familia yetu... Hatuna cha kuwalipa ila tutawakumbuka katika Sala kila mara ili Mungu awaongezee moyo huo na kuwafanikisha katika malengo yenu. Mungu awabariki sana!.
Pili kuhusu afya yangu bado kifua hakijaimarika sawa sawa na Kesho inawezekana nikahamishiwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya vipimo na matibabu zaidi (Kipimo cha CTScan hapa KCMC ni kibovu)...
Mwisho napenda kuwahakikishia wanaRombo kuwa waondoe hofu, Kamanda wao kwa hali niliyo nayo inavyozidi kuimarika ninatarajia kuwepo kwenye bunge la Budget kwa ajili ya kuwawakilisha kikamilifu.
Ahsanteni sana,
Mungu awabariki.
Joseph R. Selasini
Mb-Rombo (CHADEMA)
Post a Comment
CodeNirvana