Loading...
Stiriti Dikishenari na Masanja Mkandamizaji anatwiiti namna hii
#StiritiDikishenari Mdananda: Kutafuta ankara hapa na pale. Hakuna kituo maalumu. Ifuate ilipo, ikamate!
#StiritiDikishenari Kimenuka: dili imeharibika, mpango umeeksipaya.
#StiritiDikishenari Simamia Shoo: lipa bili.
#StiritiDikishenari Tukisanue: Tuondoke zetu. Likitumika TMK lina maana tofawuti kabisa kabisa!
#StiritiDikishenari Twira: Mahali popote unapomkuta kiongozi mkubwa bila eskoti, wala vii eiti.
#StiritiDikishenari Nimesanda: mambo yameenda ovyo! Pia "Ua Bendi" kule TMK na Tandale. Siko Poa maeneo ya Sinza. Njoo Kesho: kwa mdosi!
#StiritiDikishenari Masabu na rii: makalio
#StiritiDikishenari Bloku Fote Wani: mtaa wowote wenye machejo (ngebe kiasi + mbwembwe za wastani + ubabe kiasi)
#StiritiDikishenari Toleo Maalumu: mbongo yoyote ambaye ukifanya naye biashara au dili anakulipa bila kuzingua kabisa.
#StiritiDikishenari Kiraka: mtu anayekukopeshaga mkwanja ukishagongea kila kila mahali ukakosa!
StiritiDikishenari Unazinguwa: Hueleweki! Nje ya mada! Temeke wanasema Chenga!
Mfuatilie kwa twitter..
Masanja Mkandamizaji @masanjawani
Post a Comment
CodeNirvana