Nora Damian
WANAUME wenye matatizo ya nguvu za kiume wameshauriwa kwenda katika kliniki za afya ya uzazi badala ya kukimbilia kwa waganga wa kienyeji. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mtaalamu wa Mambo ya Jinsia na Afya ya Uzazi, Cuthbert Maendaenda alisema kuwa asilimia 60 ya wanaume wana matatizo ya nguvu za kiume nchini.
Alisema kuwa wanaume wengi wanakabiliwa na msongo wa mawazo uliowasababishia matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Mtaalamu huyo alikuwa akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu Mradi wa Ushiriki wa Wanaume Kwenye Afya ya Uzazi (TMEP), unaotekelezwa kwa ushirikiano na Chama cha Afya ya Uzazi na Ujinsia cha nchini Sweden (RFSU).
“Tiba yake ni ushauri nasaha, ambayo utaipata kwenye kliniki ya uzazi. Wanaume wenye tatizo hilo wasikimbilie kwa waganga wa kienyeji,”alisema Maendaenda. Alitaja mambo mengine yanayosababisha tatizo hilo kuwa ni magonjwa ikiwamo kisukari, shinikizo la damu, kifua kikuu, magonjwa ya ngono, Ukimwi na umri mkubwa.
Alisema asilimia 50 ya matangazo ya tiba za asili nchini yanahusu tiba ya nguvu za kiume na kuongeza kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya tendo la kujamiiana na kula karanga ama kunywa supu ya pweza. Mratibu wa mradi huo, Arthur Mtafya alisema unatekelezwa katika wilaya sita za mikoa ya Singida na Rukwa na kwamba ulianza mwishoni mwa mwaka 2010.
Mwananchi.
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana