Asali mbichi, ile nzuri kabisa ambayo haijachakachuliwa inao uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo. Kama ujuavyo asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kuna kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho kama ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo. Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni.
Lamba vijiko vikubwa viwili kila siku asubuhi mapema tumbo likiwa tupu. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo.
Lakini ili asali ifanye kazi vizuri zaidi, unahitaji iwe imechanganywa na mdalasini, na zifuatazo hapa chini ni faida 27 za asali iliyochanganywa na mdalasini.
Asali na Mdalasini
Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali.
Sasa hivi kuna makala nyingi zilizo andikwa zikielezea kuhusu uwezo wa asali katika tiba ya magonjwa mbalimbali.Warusi na Wafaransa wanafahamika sana katika kufanya utafiti katika maabara kuhusu uwezo wa asali katika tiba mbalimbali.
Katika makala hii tutaangalia tiba ya asali na mdalasini na namna ya kuitumia kutibu maradhi mbalimbali (asali tunayoizungumzia hapa ni asali safi yaani asali mbichi ya nyuki wakubwa na wadogo).
YAFUATAYO NI BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIKA KWA ASALI NA MDALASINI:
1. Ugonjwa wa viungo, maumivu na uvimbe
- Chukua maji kiasi vuguvugu na ongeza mdalasini, unga kijiko cha chai na asali vijiko 2 vya chakula na kuchua sehemu zenye maumivu.
-Vilevile waweza kutengeneza kikombe kimoja cha chai kwa kuweka kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na kuongeza asali vijiko viwili vya chakula na kisha kunywa ikiwa ya moto kutwa mara mbili.
2. Kukatika kwa nywele
- Asali ikichanganywa na mdalasini na mafuta vuguvugu ya mzeituni hutia kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele.
- Tumia mchanganyiko huo vuguvugu kwa kupaka na kusugua kichwani na acha kwa dakika 15 kisha uoshe.
3. Ukungu wa miguu au fungus
- Changanya kijiko cha chakula cha asali na vijiko viwili vya chai vya mdalasini na acha kwa muda wa nusu saa kisha safisha (rudia hivyo mpaka upone).
4. Maambukizi kwenye kibofu cha mkojo
- Changanya maji ya uvuguvugu na vijiko 2 vya chai vya mdalasini na kijiko1 cha asali huondoa bakteria kwenye kibofu.
5. Maumivu ya jino
- Changanya sehemu tano za asali na sehemu moja ya mdalasini na dondoshea kwenye jino linalouma hadi maumivu yatakapotoweka.
6. Vidonda vitokanavyo na magonjwa ya kulala kwa muda mrefu
- Paka saladi iliyochanganywa asali na mdalasini.Vilevile tumia chai ya roseberry nyekundu kwa kuondoa aina hii ya maumivu.
7. Lehemu
- Changanya asali safi mbichi vijiko 2 vya chakula na unga wa mdalasini vijiko 2 vya chakula na kikombe cha chai cha maji ya moto na unywe kutwa mara 3
8. Mafua
- Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali vuguvgugu na robo kijiko cha unga wa mdalasini kuondoa chafya na kuvimba koo.
9. Ugumba
- Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi. Wapenzi wa jinsia zote wanashauriwa kunywa walau vijiko 2 vya chakula kila siku kabla ya muda wa kulala. Mdalasini imetumika muda mrefu katika dawa za kichina na kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa
- Changanya mdalasini na kiasi cha asali na kufanya mgando (paste) na upake kwenye fizi na meno na kuacha inyonywe na kuingia mwilini taratibu na hii ni kwa akina mama wasio na sababu za kimsingi za kuwakosesha kuzaa.
10. Mchafuko wa tumbo
- Asali kwa muda mrefu imetambulika kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali pia hupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
11. Gesi au Asidi
- Kula asali pamoja na mdalasini kuondoa mchafuko wa tumbo uletwao na gesi (acid) na huu ni uchunguzi ulio fanywa na Japan na India
12. Ugonjwa wa moyo
- Unaweza kujikinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara kwa kupakaa kama jam wakati wa kula mkate wa ngano wenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko 1 cha chakula cha mchanganyiko huo (asali na mdalasini) kila siku.
13. Shinikizo la juu la damu
- Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya kupata dozi ya mara kwa mara ya asali iliyochanganywa na mdalasini.
14. Kinga ya mwili
- Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja. Utafiti unaonyesha kuwa hazina kubwa ya vitamini (virutubisho), madini pamoja na mchanganyiko wa mdalasini na asali iondoayo magonjwa na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za damu husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea na bakteria.
15. Ukosefu wa nguvu za kiume
- Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu ya uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji. Asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za mashariki za dunia. Watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali inauwezo wa kupelekea mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo mdalasini.
- Katika Afrika na dunia ya kusini mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza nguvu ya kufanya mapenzi.
16. Matatizo katika mmeng’enyo wa chakula
- Kula vijiko 2 vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo huondoa kiungulia na wataalam wanasema asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa chakula tumboni na mdalasini unaongeza kasi ya kuchaguliwa kwa chakula.
17. Flu
- Tafiti moja ya Kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa iliyopo katika asali ni dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu vimelea(virus)waletao flu.
18. Kuongeza umri wa kuishi
- Unaweza kuishi hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali.
Kutengeneza kinywaji hiki kitamu weka vijiko 4 (vikubwa) vya mdalasini na vijiko 4 vya asali,vikombe 3 vya maji na koroga kwa dk 10 kisha kunywa robo kikombe mara 3 au 4 na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.
19. Kuondoa chunusi
- Changanya vijiko 3 vikubwa vya asali na kijiko 1 kikubwa cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.Uwezo wa asali wa kuua bakteria unafanya uso kuwa wa kawaida katika muda wa wiki 2.
20. Kuumwa na wadudu wenye sumu
- Changanya asali na mdalasini kisha pakaa moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia tena hadi uvimbe uishe.
21. Maambukizi katika ngozi
-Fanya kama ilivyoandikwa namba ishirini hapo juu.
22. Kupunguza uzito.
- Waweza kufurahia vyakula vyote unavyovipenda kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri kilichojaa vitu muhimu viwili ambavyo ni asali na mdalasini.
- Unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako.Vilevile wataalam wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyama nyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko 2 vikubwa vya asali na kijiko 1 cha mdalasini.Rudia mchanganyiko huo kabla ya kulala.Wataalam wamethibitisha kuwa inapunguza hamu ya kula na kuleta joto mwilini.
23. Saratani
-Utafiti uliofanyika huko Australia na Japan umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya magonjwa kwa anaetumia madawa ya kutibu saratani. Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua saratani ya mifupa na utumbo ambao walikuwa wanatumia kila siku dozi ya asali na mdalasini walionyesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wanatumia madawa ya kutibu saratani peke yake. Dr.HIROKI OWATA alisema waliwapa mchanganyiko wa asali na mdalasini kijiko kimoja kutwa mara 3 kwa mwezi 1 na wengine waliendelea kama kawaida.
24. Kuondoa uchovu sugu
- Uko ushahidi kwamba sukari asilia iliyopo katika asali inauwezo wa kuongeza nishati mwilini. Ikitumika ipasavyo sukari hii inaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.Wataalam wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu kikombe cha maji yaliyonyunyiziwa mdalasini kunywewa masaa mawili baada ya kuamka.
Rudia kunywa saa 9 alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kuisha kufuatia ushauri wa Dr. MILSTON ABBOZZA ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.
25. Kuvimba nyayo
- Changanya asali na mdalasini katika maji vuguvugu na uchue miguu(nyayo)zilizoathirika baada ya siku ndefu ya kazi au baada ya mazoezi marefu.Rudia kila asubuhi na unawe nyayo kwa maji baridi na vaa viatu.
26. Harufu mbaya mdomoni
- Chukua maji ya vuguvugu changanya na asali na mdalasini kisha sukutua kila asubuhi.Katia Asia ya kusini mashariki watu hula kijiko cha asali na mdalasini ili kuondoa harufu mbaya(halitosis).Wataalam wanaamini uwezo wa kuua bakteria uliopo kwenye asali ndio unaopigana na harufu mbaya toka mdomoni.
27. Kupungua kwa usikivu
- Dozi za kila siku za asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu kuwa makini kama ilivyogunduliwa na Wagiriki zamani.
- Kutumia mdalasini na asali kutakufanya uonekane kuwa na afya nzuri.
Hata hivyo aina ya mdalasini unaotumia pia inahusika katika kutibu vidonda vya tumbo au maradhi mengine. Nashindwa kupata maneno haya kwa Kiswahili lakini kuna aina kama mbili hivi za mdalasini ambazo ni ‘Cassia cinnamon’ ambao wenyewe huwa na kitu kingine ndani yake kiitwacho ‘coumarin’ ambayo ni sumu na husababisha matatizo katika ini. Mdalasini nzuri kwa kutibu kisukari na ambayo bei yake ipo juu kidogo ni ile iitwayo kwa kiingereza kama ‘Ceylon cinnamon’.
Angalizo kuhusu Asali feki
Ndugu msomaji napenda kukufahamisha kuwa miaka ya karibuni kumejitokeza baadhi ya wafanyabiashara kutengeneza asali feki kwa kutumia maji ya miwa na sukari guru au kuongeza maji na vimiminika vingine ndani ya asali ili wajipatie faida kubwa, endapo utatumia asali ya namna hii basi utakuwa ukiihatarisha afya ya mwili zaidi badala ya kujitibu.
Zifuatazo ni mbinu za kuitambua asali ambayo ni salama kwa maana ya kwamba haijachakachuliwa:
• Weka maji kwenye glasi na kisha mimina asali ndani yake na kwamba ikikaa chini ya glasi bila kuchanganyana na maji basi hiyo ni asali asilia na inakuwa haijachanganywa na chochote.
• Njia ya pili ni kuiweka asali kwenye njiti ya kibiriti na kisha kuiwasha ikiwa njiti hiyo itawaka basi asali haijachakachuliwa kwa kuchanganywa na chochote lakini njiti ya kiberiti isipowaka inakuwa ni feki.
• Njia nyingine ni kuionja bidhaa hiyo na kwamba iliyokachuliwa kwa kuchemshwa hutoa harufu ya moshi tofauti na ambayo ni halisi.