Baada ya Shilole kudai kuwahi kushawishiwa kujihusisha na biashara ya
madawa ya kulevya katika muziki wake, mpenzi wake Nuh na yeye amekiri
kukutana na changamoto hiyo hiyo.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Nuh alisema kama angekuwa anataka mafanikio ya haraka angekuwa ameshapotea.
“Wengi waliokuja walikuwa wananiambia issue za kuuza madawa ya kulevya, nianze kusafiri ili niweze kupata pesa ya kuendeleza muziki wangu,” alisema Nuh.
Aliongeza, “Mimi ni mwanaume niliyekamilika na nilichagua kuishi katika maisha yangu, sikuchagua maisha ya kuuza madawa ya kulevya, nimechagua maisha ya kuishi mimi ni mwanamuziki na kupata pesa kupitia muziki wangu. Kwahiyo maisha pia ni chaguo lako wewe mwenyewe ambaye unaishi. Kama umechagua kuishi maisha yako kwa shortcut utapata vitu kwa shortcut na maisha yako yatakuwa shortcut vile vile.”