NYOTA wa Hip Hop Bongo kutoka Kundi la Weusi,
Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ ameibuka na kuwapa somo vijana kwamba
wanatakiwa kutumia changamoto wanazopitia katika maisha na kuwa
mafanikio kuliko kukaa na kulaumu.
kipiga
stori na Risasi Vibes, Nikki wa Pili anayebamba na Ngoma ya Baba
Swalehe alisema, vijana wengi wamekuwa na dhana kwamba wakishasoma
wanategemea kuajiriwa tu kitu ambacho siyo kizuri na kinaweza
kuwagharimu kwani ajira kwa hapa nchini zipo chache hivyo ni vyema
wakatumia changamoto za ajira kuwa mafanikio kwao.
“Vijana tunatakiwa tuamke hata kama umesoma mpaka wapi usitegemee
kuajiriwa tu kwa sababu utaishia kukaa kijiweni ukisubiri ajira na
mwishowe unakuwa muhuni wa mtaani, ni vyema tukajiajiri wenyewe hiyo
itatusaidia kuendesha maisha yetu ya kila siku,” alisema Nikki wa Pili.