Nay Ameachia Wimbo Mpya na kusema kuwa aliyoyazungumza humo ni mambo ambayo yapo na huenda tunayajua au tumesha yasikia mitaani.
Katika moja ya mistari yake amemzungumzia Rais John Pombe Magufuli na kusema kuwa kama watu watamzingua avunje mpaka Ikulu
Miongoni mwa vijembe vinavyopatikana kwenye wimbo huo ni;
Msanii Ray kujifanya Mkongo kwa kununulia mkorogo fedha zinazotokana na mauzo ya movie zake na kuishi kwao hadi sasa, Bongo Movie imekufa kufikia hatua wasanii wa kike wa filamu kutaka kuimba km snura na shilole, Niva kuishi kwa mademu na huku akimiliki gari ya M10 wakati hana getto, wanafunzi wa chuo kuishi maisha ya anasa na kupoteza dhana ya usomi. Wadada wengi wa mjini na kutovaa chup**, biashara?
Hakuishia hapo, alihamia kwa BASATA, kwa kuwashangaa wanavyoshindwa kufanya kazi yao kwa weledi na kuishia kuwafungia wasanii nyimbo bila kujua ugumu wanaopitia..
Pia, akaendelea na wadananda kwa kumtaja Shetta kuwa anaringishia gari ya kifahari aliyohongwa na Chief Kiumbe kwa kujitapa 'My new ride', Ommy Dimpoz kuhusishwa na Ushoga kitaani, DJ Choka kuwa bize na bata bila kujali familia huku hana hata godoro la kulalia.
Katika wimbo huo Nay wa Mitego hajamuacha Wema Sepetu na alikuwa na haya kusema juu yake " Wema Sepetu una mimba kweli kweli au unatafuta kiki za msimu, miezi tisa si mingi isije ikakugharimu, na anamshauri aangalie umri unaenda asiendekeze kiki kwani mwishowe ataitafuta Kiki hadi kwa FID Q. "
Hata hivyo baada ya Nay wa Mitego kuachia wimbo huo amesema maneno haya "Hii sio Vita japo inaweza kua vita. Ni muziki mzuri na mtamu sana wenye maneno flani ya wazi tu ata wewe unayajua.! #ShikaAdabuYako nitaenda likizo kidogo baada ya hii Ngoma kuanza kuchezwa." Aliandika Nay wa Mitego

"Mliopanga kunishtaki mkanishtaki hata kwa Magu na bado nitawapa fact, si wamekuchagua wenyewe Magufuli waonyeshe maujuzi vunja mpaka Ikulu wakikuletea upuuzi, sifanyi bifu mimi na watoto wa juzi" Asema Nay