Mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Mike Mwakatundu ‘Mike Tee’.
Mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Mike Mwakatundu ‘Mike Tee’
amesema alikuwa kimya kwa muda mrefu kwa vile alikuwa analisoma upya
gemu kwani kuna mabadiliko makubwa katika tasnia hiyo kwa sasa.
Alisema fleva za sasa zimebadilika hivyo ni jambo zuri kwa msanii
kulifahamu vyema soko la muziki linataka nini na ili iwe hivyo, yampasa
kurudi nyuma, kukaa kimya na kuwasoma mashabiki ili kujua wanahitaji
nini toka kwake kabla ya kutoa kazi.
“Mimi nawakilisha watu wawili, Mike Tee msanii na Mike Mwakatundu
kama taasisi, ilifika sehemu Mike Mwakatundu ilibidi naye apewe nafasi
maana ni baba wa watoto wawili (Michael and Michelle) na ni baba wa
familia so kuna mambo ilibidi kuyaweka sawa ya kifamilia ili niweze
kujigawa vizuri upande wa muziki na maisha ya kawaida,” alisema Mike Tee
ambaye amerejea kwa kishondo na kibao chake cha Kiduchu