STAA
wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana
amemwangukia kwa mara nyingine aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed
‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika wakati mgumu
tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na
kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao
kama ilivyokuwa zamani.
“Ndugu
yangu nikikwambia kuwa, Nuh maji yamemfika shingoni basi huna haja ya
kuuliza mara mbili namna yalivyomfika kwani, juzikati nilikuwa naongea
na Shilole akalalamika kwamba, jamaa huyo ameanza tabia ya kumpigiapigia
simu akimwomba warudiane jambo ambalo Shilole analitolea nje,” kilisema
chanzo hicho.
Baada
ya kupenyezewa ubuyu huo, paparazi wetu alimtafuta Shilole kwa nia
njema ya kutaka kujua ukweli wa madai hayo ambapo alisema ishu hiyo ipo
ila hawezi kuanika wazi.
“Suala
la Nuh kwa sasa sitaki kuendelea kuongea kwani nitakuwa nampigia debe
mtu na kazi hiyo niliifanya sana. Unachotakiwa kujua kutoka kwangu ni
kwamba mimi naendelea kupigania maisha tu ili niweze kusonga mbele na
hapa nipo kipesa zaidi hivyo sina tena muda wa kuendelea kumpa nafasi
bwana wa aina yeyote kwani hapo nyuma maisha yangu yalirudi nyuma hatua
nyingi sana,” alisema Shilole.STAA wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari
Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana amemwangukia kwa mara nyingine
aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika wakati mgumu
tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na
kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao
kama ilivyokuwa zamani.
“Ndugu
yangu nikikwambia kuwa, Nuh maji yamemfika shingoni basi huna haja ya
kuuliza mara mbili namna yalivyomfika kwani, juzikati nilikuwa naongea
na Shilole akalalamika kwamba, jamaa huyo ameanza tabia ya kumpigiapigia
simu akimwomba warudiane jambo ambalo Shilole analitolea nje,” kilisema
chanzo hicho.
Baada
ya kupenyezewa ubuyu huo, paparazi wetu alimtafuta Shilole kwa nia
njema ya kutaka kujua ukweli wa madai hayo ambapo alisema ishu hiyo ipo
ila hawezi kuanika wazi.
“Suala la Nuh kwa sasa sitaki kuendelea kuongea kwani nitakuwa nampigia debe mtu na kazi hiyo niliifanya sana.
Unachotakiwa
kujua kutoka kwangu ni kwamba mimi naendelea kupigania maisha tu ili
niweze kusonga mbele na hapa nipo kipesa zaidi hivyo sina tena muda wa
kuendelea kumpa nafasi bwana wa aina yeyote kwani hapo nyuma maisha
yangu yalirudi nyuma hatua nyingi sana,” alisema Shilole.
Chanzo:GPL