Wachezaji wa timu ya Azam FC hivi sasa wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA), tayari kabisa kwa safari ya
kuelekea jijini Johannesburg Afrika Kusini saa 4 asubuhi leo kucheza
mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi
ya Bidvest Wits ya huko.
Mchezo huo utafanyika Jumamosi ijayo (Machi 12) katika Uwanja wa
Bidvest kuanzia saa 1.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na kikosi
hicho kimeondoka na morali kubwa kabisa ya kupata matokea mazuri ugenini
baada ya kufanya maandalizi ya kutosha.