Wanasema hela zinaenda kwa wale ambao tayari wanazo. Kwa Diamond kuamka na dili mpya kila kukicha kimekuwa ni kitu cha kawaida.
Na
sasa staa huyo amesaini mkataba wa ubalozi wa tomato sauce tunayokutana
nayo mara kibao kwenye vile vijiwe vya kulia viepe, Red Gold.
Amesaini mkataba huo jana kwenye ofisi zake za WCB. Huo ni mkataba wa tatu baada ya DSTV, Vodacom.