Mbio za ubingwa wa Ligi maarufu zaidi duniani ya EPL zinaingia katika hatua tamu sana baada ya hapo jana Tottenham kupunguza pengo la pointi na vinara wa ligi hiyo Leicester City na kufikia pointi tano baada ya kuifunga Stoke City bao nne kwa bila.
Mshambuliaji
wa Tottenham Hotspur, Harry Kane na Dele Alli ndio walikuwa mashujaa jana baada ya kuifungia mabao mawili timu yao katika ushindi wa
4-0 dhidi ya Stoke City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa
Britannia.Sasa timu
hiyo inafikisha pointi 68 baada ya kucheza mechi 34 na kuendelea kukaa
nafasi ya pili nyuma ya Leicester City yenye pointi 73 za mechi 3.
CHANZO:Daily Mail