Ukiamka asubuhi vituoni mwa daladala utawakuta vijana wakiwa na sarafu mkononi kama vile wanazigawa vile? lakini huwakimbilia makonda na huku wakiwauliza iwapo wanahitaji kumbe wanawauzia.Kama konda anashida na sarafu hizo ili awarudishie abiria wake na hana mfukoni mwokozi wake ni hawa jamaa ambao sijapata jina lao wanaloitwa kama wengineo walivyo maarufu.
Lakini hali hii ni kuwa ni kukua kwa uchumi au hali ya maisha inazidi kubana?
Hawa jamaa ukiwauliza wanadai ni biashara nzuri tu kwani hawezi kukosa pesa ya kula kwa siku.
Ukipita kuanzia TAbata shule,Buguruni Rozana,Boma sokoni, MIkumi magomeni kutawakosa hawa waheshimiwa.
Naweza kumpongeza aliyeanzisha hili wazo kwani alikaa chini akawaza na kupata jibu muafaka
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana