Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Ungekuwa wewe ungeamua lipi?

Kumezuka minong'ono ya hapa na pale kuhusiana na ujio wa waliokuwa Mabingwa wa ulaya timu ya Real Madrid.Timu hii itakuja nchini katika kipindi cha maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya kwa ligi yao La liga.
Kuna washika dau ambao wanadai timu kuileta hapa nchini ni kazi kutokana na sababu kuwa
Kwanza,timu hii haitazisaidia lolote timu za hapa nchini kwani hata wakicheza nao viwango vya timu hizi za bongo havitakua.
Pili, ni ghali mno kuileta timu hii hapa kwetu ukizingatia tuna matatizo lukuki.Hapa hata waheshimiwa wenyewe waliweka wazi kuwa huu mzigo serikali inahitaji washika dau watie mkono.
Watu mbalimbali wapendeza kuwa kama serikali inahitaji soka likue hapa bongo dawa sio hiyo ya kumleta Cannavaro,bali ni kutafuta vijana wadogo wa umri wa miaka 16 na 17 hawa wapelekwe Ulaya au Brazili wakafuliwe ili baada ya muda warudi wakiwa wamefundishwa mbinu mbalimbali.Japani waliwahi kufanya hivi na tumeona sasa wanatmba Asia na hata Ulaya wapo wachezaji wanasukuma soka kule.
Pia tuna Uchina hivi karibunin tuliona vijana wa timu ya olimpiki wa china waliokuwa Uingereza kwenye vituo vya michezo wakifundisho soka.wana jiandaa kwa ajili ya michezo ya OLimpiki itakayo fanyikia China ili wasijetia aibu.
Hawa wenzetu wanaangalia mbali.
Tunahitaji maamuzi yenye tija ili soka la bongo nalo likue ili kule Kijiweni Rundugai tujazane kumwona Steven Gerard wa Bongo.
Mpo hapo
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top