Zamani enzi zile za Kichwa cha Mwendawazimu ni kuwa tukipigwa goli kesho yake ni wimbo kila baya litasemwa kidogo hali hii imebadilika toka tumegaragazwa 4.0.
Kuna mdau mmoja akachomekea unajua kaanzaje,.......
....Kuwa inaelekea mteule wetu yaani kocha wa staazi ni mwoga wa mechi kubwakubwa za majaribio,ndio maana akawa anachagua mechi kipindi ambacho sivyo kalenda ya FIFA inavyo longa.Duu hapa simo.
Lakini ni kweli ?
Hebu tuangalie kidogo,Tulicheza na Angola,DRC Congo.
Timu hizi wanadai ziliwaleta wachezaji wa ligi ya pale pale ktk miji mikuu yao yaani Luanda na Kinshasa.So wale wenyewe wakandamizaji kama Masanja Mwafrika anavyosema.
Tukawa piga bao nasi tukafurahi Kocha nae liCV likawalinameremeta.
Jamaa anasema yote hayo yalitufanya twende Dakar tukijua tunaenda kushinda kumbe sio mwisho wa yote tukaonekana kuwa tu wepesi hatuna stamina pamoja na Kuogelea pale Copa Kabana.
Hii ni changamoto kwetu kwani tumepata somo.
Ni tumaini langu kuwa viongozi watakuwa wameona makosa mengi tu pamoja na kuwa hawatasema lakini mojawapo ni hili,
Pamoja na kuwa kocha anakuwa na programu yake ambayo ni dira kwa maandalizi ya mechi au mashindano mbalimbali ni vema WAkuu wa chama chetu cha mpira wa miguu wakawa nao waitathimini programu hiyo ili nao waone kama inaweza kutusaidia.
Huu mtindo wa kucheza mechi ambazo hazitaisaidia timu tumeanza kuona matunda yake. Hatukuona sifa za watu uwanjani wale wenye mashutio hatukuyaona,wale winga terza walikuwapo?
Pia tetesi hizi za kuwa huyu mtaalamu ndio mwisho wa kila kitu akisema yeye ndio basi zinakera zinahitaji majibu ya HARAKA ili tujue ni kweli?
Wadau sasa wanashanga au ndio maana tulijitoa chalenji ili ubovu wetu usionekane tukapeleka vijana mseto ?
Nne ni nyingi jamani zinauma.
Pamoja na kuwa tunamechi zinakuja yabidi tuangalie na soka la Vijana kwani kuna mashindano mengi yanakuja tutafute chipukizi wapya hawa huenda ndio mwisho huo.
Kwa kweli walijitahidi lakini uwezo wao umefikia hapo.
Tutafute vijana wanaowaza kwenda kusakata ulaya hawa walikuwa wanawaza simba nayanga hivyo wamefika wanaona ndio mwisho hebu tulete damu mbichi.
Tunahitaji mabadiliko ili nasi tucheke nne mpaka lini.........????????
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana