Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Una soni ?

Rafiki yako au ndugu yako unapomwalika kuja kwako baada ya wewe kumtembelea kwake unajitahidi sana kusafisha pale kwako kwa ajili ya ugeni huo ili akija japo urithike kuwa ameona kuwa unakaa sehemu safi na inayovutia au tunaweza kusema sehemu nzuri.
Hii yote ni kuwa binadamu tuna aibu.Unaona aibu kuwa asije kukuta nyumba au chumba unachokaa ni pa chafu.
hapa tunajitahidi kwa bidii zote kuhakikisha kuwa panapendeza japo kwa muda ule ambao mgeni au ugeni ule utakuwa pale,sote haya ni mambo ya kawaida kwetu mimi na wewe.Ndivyo tunavyoishi.
huwezi kwenda kwa ndugu au rafiki ukakuta kwake kuna vutia halafu anapokuja kwako upaache kama palivyo ni kuwa utajitahidi nawe kwako japo kwa muda ule mgeni huyo aone kuta zinapendeza baada ya wewe kuzisugua chumba umepanga vizuri na sebule pia kama ipo.
Lakini najiuliza sana sipati jibu,
Watu mbalimbali katika nchi zetu hizi wamekuwa wanasafiri sana kwenda kwenye nchi za ulaya na america huko wanakuta miji iliyopangiliwa vizuri na inapendeza sana kiasi kwamba nao wanaona fahai kuwapo pale.Uzuri huu ni kuwa wenzetu waliandaa miji yao ndio ikawa hivyo.
cha kushangaza zaidi ni kuwa hakuna hata moja waliloliona huko na kuja nalo hapa au niseme kuwa hawaoni aibu kuwa wanakuta huko kunapendeza sana lakini wakija hawachukui hatua za kupaboresha kwao.
Unaweza kuyaona haya hata katika mitaa mbalimbali,utakuta mtu kaporomosha bonge la Ghorofa lakini angalia barabara iliyopomtaani kwake hapo ni makorongo.
nyumba ni nzuri lakini pa kupita ni kituko.
Angalia Kariakoo mvua kidogo madimbwi miezi miwili na zaidi.
kwa wale wenzangu mnaosafiri nje anagalieni Viwanja vya ndege vya huko mnakoenda au mlipo mlinganishe na vyetu halafu mnipe jibu.
Ni kuwa mbona hatuoni aibu ?
Karibu kijiweni
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

4 maoni

hii sasa kali waRundugai.

Reply

Aibu kitu cha ajabu!Mkiwa wengi ni rahisi kukiua na kuona yale ya aibu kawaida. Nafikiri ushasikia msanii wa picha ambaye hupenda kupiga makundi ya watu sehemu za wazi kwa kisingizio cha usaniii. Wanaojitolea kwenye picha zake wanadai kuwa ni watu wenye aibu, lakini kwa kuwa kundi zima linavuanguo kwa pamoja katikati ya mji , basi hata mwenye aibu anajisikia poa tu. Naamini wengi wasafirio, wakirudi bongo wanafanya mambo kama wabongo au wa pale mtaani wafanyavyo,kwa kuwa ni rahisi, yakiwashinda wanaanza tena nje ya nchi.

Lakini naamini tunahitaji viongozi wa kuonyesha mfano hasa kwa wale waliona na wanaojua jinsi ya kufanya mambo yawe bomba.

Lakini ...
Una soni, ni kiswahili au kipare?:-)

Reply

Hii ni balaa. Ujumbe wako ni wa kweli na hata mimi huwa inaniuma kweli. wananchi hatuoni na viongozi hawaoni. ni balaa tupu.

kazi kwetu. tunaweza kulipigia debe au tukaacha pasiwepo mabadiliko. Ila nafikiri kuna haja ya kuingia bungeni hata kwa mlango wa nyuma na kuwaambia wabunge wafanye kazi. kwa heri mwanawane ngoja nikandamize kazi kidogo hapa

Reply

Ni kweli kuwa unaweza kuona aibu iwapo utalinganisha mwenzako/jirani/rafiki yako pake pamependeza na kwako ku hoi bin taabani!

Ukweli wenyewe katika suala la kupanga mji yetu, tumetohoa kila kitu toka kwa mkoloni wetu, aidha sio sahihi kusema kuwa hatuna aibu. Mfumo wetu ndio umetufikisha hapa tulipo, ambapo kumekuwepo na ongezeko kubwa la ujenzi holela. Hii imechangiwa na ongezeko kubwa la wahamiaji katika miji yetu mikubwa, huku vyommbo husika vikishindwa kukidhi haja ya wahamiaji hao.

Pamoja na yote hayo, wapo wananchi ambao hata hawajawahi kusafiri nje ya nchi na kujionea jinsi miji ya huko ilivyopanga, lakini kutokana na athari za kujenga holela wamejifunza, na sasa wapo na wanaendelea kurekebisha maeneo wanayo ishi. hapa chini nina mifano hai ya Watanzania ambao wamesema basi kuishi kienyeji...!

Hananasif: Ipo katika halmashauri ya jiji la kinondoni, baada ya kuvamia eneo hilo na kujenga pasipo mpango, wananchi wa kitongoji hicho, waliamua kwa pamoja kurekebisha miundo mbinu ya kitongoji hicho. Uwamuzi wao umewasaidia sana kwani sasa hawana tena tatizo la mitaro ya maji machafu na mvua. Barabara zimeongezwa upana ingawa sio katika kiwango cha lami.

Iringa:
Kuna kitongoji kimoja mkoani hapo, kiliamua kujenga barabara za kupita magari, na ni baada ya kuona kuwa wanapata shida kubwa ya usafiri kutokana na kujenga kiholela. baadhi ya wananchi kwa hiari yao walikubali kuvunja nyumba zao ili kuweza kupatikana kwa barabara. Zaidi waliweza kujenga nyumba bora kwa ajili ya wajane kibao waliokuwepo katika kitongoji chao.

Maili Nne- zanzibar:
Wananchi wa kitongoji hichi waliamua wenyewe kujipangia namna ya ujenzi wa nyumba zao, ingawa bado kutambuliwa na serikali. Ujenzi wao umefuata taratibu zote za kimakaazi, tatizo tu ni kuwa wamevamia eneo hilo.

Hivyo basi aibu tunazo na si lazima mpaka tusafiri... Ni sisi wenyewe kukubali kuwa hatuwezi kuishi ovyo ovyo then kila kitu kitakuwa sawa...

Reply
CodeNirvana
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top