WITO umetolewa kwa wananchi mkoani Manyara kuepuka matumizi ya dawa na vipodozi vilivyopigwa marufuku ili kukwepa magonjwa mabaya yakiwemo ya saratani ya
ngozi na ugumba.
Hayo yalisemwa na Ofisa Afya wa Mji mdogo wa Mererani wilayani
Simanjiro, Jovin Rweyemamu wakati akizungumza kwenye kikao cha mamlaka ya mji mdogo
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mamlaka hiyo.
Alisema serikali imekuwa ikitoa elimu kupitia vyombo mbalimbali vya habari
runinga, redio na magazeti ili wananchi watambue madhara ya vipodozi vilivyopigwa marufuku.
“Ni kosa la jinai kutumia au kupatikana na dawa au vipodozi vilivyoisha muda
wake, kwani madhara yake ni makubwa kwa jamii na hata wakati mwingine watumiaji wanapoteza maisha”alisema Rweyemamu.
“Faini kwa mkosaji ni Sh 1 milioni au kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja na hii ni kwa mujibu wa sheria ya vyakula dawa na vipodozi ya mwaka 2003,”alisema Rweyemamu.
Alidai kuwa dawa na vipodozi vilivyopigwa marufuku vinasumu hivyo vinapotumika
huathiri ngozi ya binadamu kwa namna mbalimbali bila wao kujijua.
Aliasa jamii nchini kuepuka matumizi ya dawa hizo ambazo wakati mwingine
Zinauzwa kwa kificho kutokana na mamlaka kuanza kuingilia kati kutaka
yateketezwe.
Chanzo:Mwananchi
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana