MAMLAKA ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imekwepa lawama ya ajali ya meli ya Mv Spice Islanders iliyotokea usiku wa kuamkia Septemba 9, mwaka huu visiwani Zanzibar. Katika taarifa yake ilitolewa kwa vyombo vya habari juzi, Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray, alisema utendaji wa Sumatra Tanzania bara hauna uhusiano wa moja kwa moja na mamlaka inayosimamia ulinzi na usalama wa usafiri majini Zanzibar.
"Meli ya MV Spice Islanders, ilisajiliwa na mamlaka inayosimamia ulinzi na usalama wa usafiri majini ya Zanzibar na inamilikiwa na Kampuni ya Alghubra Shipping, inayomilikiwa na Salum Said Batwash,” inasema taarifa ya Sumatra na kuongeza:
"Hivyo shughuli za usimamizi na udhibiti wa usafiri wa majini katika Mamlaka ya Usafiri wa Majini kwenye visiwa vya Unguja na Pemba, zinasimamiwa na Sheria ya Usafiri Majini ya Zanzibar ya 2007 siyo Sumatra kwa upande wa Tanzania bara, ambayo inatumia sheria ya mwaka 2001.”
Taarifa hiyo inasisitiza: ” Sheria ya Usafiri wa Majini ya Zanzibar, imetoa jukumu la kusimamia usafiri wa majini katika Mamlaka ya Usafiri wa Majini ya Zanzibar inayojulikana kama Zanzibar Maritime Authority.
Kutokana na tukio la ajali hiyo, Mamlaka ya Usafiri wa Majini ya Zanzibar ndiyo yenye jukumu la kuwa msemaji na mtoa taarifa wa shughuli za uokoaji. "Kwa maelezo hayo, wote wenye kutaka maelezo au taarifa zozote kuhusu tukio hili au masuala ya usimamizi wa usafiri na udhibiti wa usafiri wa majini kwa upande wa Zanzibar, wawasiliane na Mkurugenzi Mkuu wa Zanzibar Maritime Authority."
Katika hatua nyingine Ibrahim Yamola anaripoti kuwa, Sumatra imekubali kuhamishia kituo cha mabasi kwenye soko la wafanyabiashara ndogondogo, eneo la Machinga Complex.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya wafanyabiashara kutangaza mgomo wa kutolipa kodi ya vizimba kama hawatatekelezewa ndani ya wiki mbili. Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa soko hilo, Teddy Kundi, alisema Sumatra wamekubali kuanzisha kituo hivi karibuni ili kutatua tatizo la wafanyabiashara waliokuwa wameomba kufanyiwa hivyo.
Teddy alisema zoezi la kuvunjwa vizimba vya wafanyabiashara ambao walikaidi amri ya Manispaa ya Ilala, iliyowataka waanze kuvitumia ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wengine waliokosa vizimba, hivyo zoezi la uvunjaji makufuli umekamilika.
Chanzo:Mwananchi
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana