Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

TBC 1 na 'Valentine Day' Isiyo na Maana kwetu.

Ndugu zangu,
Nilikaa kuangalia taarifa ya habari kwenye TBC1 leo saa mbili usiku. Kwa mshangao mkubwa, nikasikia cha kwanza mtangazaji Grace Kingalame akituambia Watanzania ni; " Leo ni siku ya Wapendanao". Sentesi hiyo haikupaswa hata kutamkwa mwisho wa taarifa ya habari.

Tunawakumbusha TBC1 , kuwa ni wengi tunaosubiri taarifa ya habari kila ifikapo saa mbili usiku. Hivyo basi, taarifa ya habari ni ' serious issue'. Si jambo la kufanyia mzaha mzaha. Valentine Day ni mzaha wa watu wa Kimagharibi. Hiyo ni siku inayotumiwa kufanya biashara. Haina maana na wala haimsaidii kwa lolote Mtanzania wa Nyarugusu au Malampaka. Na wala si utamaduni wetu. Vingine si vya kuiga.
Maggid Mjengwa,
Iringa.

KUTOKA:mjengwa blog.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top