Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Chama Cha Mapinduzi kimeunda Mkoa maalum wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeunda Mkoa Maalum wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kufanya uteuzi wa makatibu tisa wa mikoa.

Makatibu walioteuliwa na mikoa yao kwenye mabano ni pamoja na;-
1. Ndg. Elikana Mauma (Mkoa wa Mara)
2. Ndg. Hilda Kapaya (Mkoa wa Geita)
3. Ndg. Shaibu Akwilombe (Mkoa wa Simiyu)
4. Ndg. Hosea Mpagike (Mkoa wa Njombe)
5. Ndg. Alphonce Kinamhala (Mkoa wa Katavi)
6. Ndg. Aziza R. Mapuri (Mkoa wa Magharibi)
7. Ndg. Maganga Sengerema (Atapangiwa kituo)
8. Ndg. Adelina Geffi (Atapangiwa kituo)
9. Ndg. Christopher Ngubiagai (Mkoa Maalum wa Wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu)

Kuundwa kwa mkoa maalum wa wanafunzi wa elimu ya juu kunalenga kupanua wigo ikiwa ni mkakati wa chama kujiimarisha zaidi kwa wanachama wake wa kada mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa elimu ya juu.
Uamuzi huu utawapa fursa wanafunzi wasomi ambao wengi wao ni vijana kupata fursa za kikatiba na kanuni kushauri na kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya ngazi ya juu katika chama cha Mapinduzi (CCM).



Nape M. Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM
Itikadi na Uenezi
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top