Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Didier Drogba kuondoka Chelsea mwishoni mwa June 2012


Didier Drogba amethibitisha kuondoka Mabingwa wa Ulaya ifikapo mwishoni mwa June wakati mkataba wake na timu hiyo utakapofikia tamati.Pamoja na kukanusha kuwa aliwaaga rasmi mashabiki wake jijini London wakati timu hiyo ilipokuwa inapita kuwaonyesha Kombe la Mabingwa wa Ulaya walilolinyakua huko Munich kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Bayer Munich leo imedhibitishwa rasmi kwenye tovuti ya Klabu hiyo Chelsea kuwa Mchezajji huyo hatakuwa na timu hiyo tena Msimu ujao na wamemtakia kila lakheri huko aendako.
Didier anaondoka Chelsea akiwa kafunga magoli 157 kwenye mechi 341 alizoichezea. Anashikilia nafasi ya nne aktika Klabu hiyo kati ya wachezaji walioifungia idadi kubwa ya magoli,akiwa na magoli 34 katika mashindano ya Ulaya.

Drogba ameshinda mataji matatu ya Ligi ya Uingereza(Barkclays Premier League),Mataji manne ya FA Cup,Mataji mawili ya Carling na Kombe la Mabingwa wa Ulaya

Tetesi zilizopo ni kuwa Drogba huenda akaelekea China na hizo bado ni tetesi tusubiri TUONE.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top