Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Ubungo yetu ilivyo leo

Kamera yetu Jumapili hii ilipitia maeneo ya Ubungo barabara ya Morogoro ambayo iko kwenye maandalizi ya ujenzi wa magari yaendayo kasi.Katika pitapita yetu hali ya Ubungo si ile tuliyoizoea ambapo pembeni mwa Barabara kulikuwa na miti iliyopamba pande zote kwa sasa miti hiyo imekata ikiashiria kazi Imeanza..
Madereva wa usafiri wa bodaboda kama uitwavyo wakiwa wamejipumzisha huku wakisubiria abria maeneo hayo ya Ubungo hali hii inaonyesha jinsi vivuli vilivyo adimika maeneno hayo.

Watu wakiwa kwenye pilikapilika zao za kila siku huku wingu zito likiwa limetanda juu angani kuashiria kwamba itanyesha si muda huku eneo hilo la Ubungo likionekana miti ikiwa imekatwa na kulifanya eneo hilo kuwa na sura tofauti kama ilivyozoeleka.

Kutokana na kuondolewa kwa machinga eneo hilo limeendelea kuwa na uwazi wa kutosha tofauti na mwanzo ambapo hali ilikuwa mshikemshike hapo huku ukimkwepa machinga na bidhaa zake chini huku guta nalo laja kabla hujasikia honi ya bodaboda mpaka uondoke eneo hilo unakuwa ushapigana vibega kadhaa.

Ni dhahiri shahiri kwamba kazi hapo imeshaanza baada ya miti iliyokuwa pembezoni mwa Morogoro Road kutolewa yote ili kupisha ujenzi wa njia ya magari yaendayo kwa kasi.

Kwa mbaali kinaonekana kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na pilika zake zikiwa zimeshika kasi.

Wengine wameamua kujitafutia riziki mitaa hiyo kama unavyowaona hao ambao walikutwa wakifukua kutafuta vyuma walivyodai wameviona na vinauzika kwa haraka sana ili waweze kwenda kwa 'Mama'.

Wahusika nao kwa upande mwingine wakiendelea na kazi zao kama kawa.




Muuza magazeti huyu aliona isiwe nongwa yeye akaamua kuweka mwavuli ili aweze kuendeleza gurudumu lake la biashara ya magazeti kama alivyodakwa na kamera yetu ya kijiweni ambayo ilipita maeneo hayo ya Ubungo na kuona hali ilivyo ambapo ile miti iliyokuwa pembezoni mwa barabara hiyo ikiwa imekatwa pupisha ujenzi wa miundo mbinu ya magari yaendayo kasi.


author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top