Loading...
Keraha za Mvua Tabata ''Tusiime''
Eneo hili liko usoni mwa shule Maarufu ya Tusiime Secondary na Msingi pia ambapo mara inyeshapo mvua eneo hilo huwa kero isiyoisha ya madimbwi makubwa ya maji hiyo ni kwa wapita njia hata magari ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo.
Kijichaka hicho kikionekana kustawi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.Hapo unaona dimbwi hilo likiweka eneo hilo kutopitika vizuri .
Gari ikitoka kuogelea kwenye dimbwi ambalo ni la tope
Taswira hiyo unaliona dimbwi mojawapo katika eneo hilo la Tusiime njia hiyo iko chini ya nguzo za kupitisha umeme mkubwa hivyo wananchi eneo hilo kushindwa kujua mwenye mamlaka ya kukarabati eneo hilo ili kuondoa maji hayo yasiwe yanatuamaa eneo hilo. Wengine wakienda mbali na kumtupia lawama mmiliki wa Shule ya kuwa kwanini hawaboreshei wateja wake eneo hilo ili liwe la kuvutia zaidi na kuondoa kero hiyo kwa wateja wake ambao wengi wao ni wale wenye kumiliki magari.
Post a Comment
CodeNirvana