Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Manchester City kuweka historia baada ya miaka 44 ya ukame .



Manchester City wanatarajiwa kuweka mwanzo mpya katika soka Ligi kuu ya Uingereza hapo kesho Jumapili kwa kutwaa taji hilo la EPL kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 44 katika mechi ya kufunga pazia dhidi ya QPR.

Timu hiy ya City baada ya kununuliwa na matajiri wa Abu Dhabi United Group imekuwa ikifanya vizuri msimu huu ambao unatazamiwa kuamuliwa kwa idadi kubwa ya magoli ya kufunga ambapo City wana idadi kubwa ya magoli zaidi ya nane kuliko waliyonayo mahasimu wao United. Matajiri hao wanatariji ona uwekezaji wao huo msimu huu unalipa kwa City kulitwaa taji hilo ambalo msimu huu limekuwa na ushindani wa hali ya juu tofauti na misimu mingine.

Ushindi dhidi ya Queens Parks Rangers hapo Eastland Jumapili utavunjwa tu na maajabu ya United kuifunga Sunderland idadi kubwa ya magoli zaidi ya tisa huku ikiombea City iteleze.

Matajiri wa City wanakisiwa kuwekeza kiasi cha Paundi 1 Bilioni kwenye Klabu hiyo ya City hivyo ushindi wa kesho ni muhimu kwa klabu hiyo na kuwa faraja pekee kwa matajiri hao wa kiarabu.

Yaya Toure,mchezaji toka Ivory Coast anaeichezea City ni mmoja wa wachezaji nguzo wa klabu hiyo msimu huu kwa kufunga magoli muhimu yaliyo iweka klabu hiyo katika nafasi nzuri msimu huu ma anamatumaini City watawika zaidi katika ulimwengu wa soka dunianimiaka ijayo.

City inasemekana wameshaanza mipango ya kusakili kwa msimu ujao wa 2012/2013 kwa kumnyemelea winga machachari wa Lille Eden Hazard pamoja na mshambuliaji mahiri Mrugwai wa Napoli Edinson Cavani.

''Ndio maana nimekuja hapa,ksaidia timu pamoja na kuwapa uzoefu wachezaji chipukizi na kuisadia timu isonge mbele na kuwa timu kubwa duniani''Alisema Toure.

''Sasa hapa tulipo tupo hatua nzuri kuweka historia tunatakiwa kushinda kitu kwa kufuata msimu uliopita tulipotwaa kome la FA''Toure aliongezea.City walifuta ukame wa kipindi kirefu wa vikombe Klabuni hapo kwa kutwaa kombe la FA.

Mahasimu wao wakubwa United wameachwa wakiiombea mabaya City ifungwe au kudroo na QPR huku nao wakitakiwa kushinda dhidi ya Sunderland ili waweze kuutwaa ubingwa huo wa EPL kwa mara ya 20.

Wakati huo QPR nao wanapigana ili kupata matokeo mazuri yatakayo wabakisha katika msimu ujao kwa kutoshuka daraja.Vita hiyo inalifanya pambano hilo la kesho kuwa muhimu sana kwa timu zote mbili moja ikitaka kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya mika 44 na nyingine ikipigania kutoshuka daraja.

City wamekuwa na msimu mzuri katiak mechi za nyumbani kwa kupoteza pointi mbili tu mpaka sasa huku QPR wakiwa na rekodi mbya kwa kupoteza mechi 13,kudroo 2 na kushinda mechi 3 za away.

Hali hiyo inaweza kusahaulika kesho wakati ambapo wanatakiwa wapambane ili waweze kukwepa kushuaka daraja huku wakiinyima City Ubingwa wa EPL.

Utamu wa mechi hiyo pia unakuja kama sehemu ya kulipa kisasi kwa kocha wa QPR Mark Hughes,ambae alifukuzwa City December 2009 katika hali ya kutatanisha hivyo kuiweka mechi hiyo kama sehemu ya kulipiza kisasi.
Lakini kocha huyo ameyapuuza mawazo hayo na kusema kwamba''Kulipiza kisasi si kitu kilicho kichwani kwangu kwa sasa,nina waza namna ya kuifanya QPR isishuke daraja''alimalizia .

Pia Mark Hughes ni mshambuliajiwa zamani wa United hivyo wengi kuona kuwa hatakubali kuwa daraja kwa kuiwezesha City itwae ubingwa kirahisi huku akiona na hivyo anatazamiwa kuleta changamoto kali katika MECHI HIYO YA KESHO.

Nani ataukwaa ufalme wa EPL KESHO ni suala la muda tu sasa.Pia nani atashuka daraja na nai pia atashika nafasi ya 3 na 4 ?

Vyote hivyo vinaifanya Ligi hiyo ya EPL msimu huu kuwa ya kipekee.Tusubiri tuone nani ni nani kesho.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top